img

Sinai Rangers watangazwa kuwa Mabingwa wa mkoa wa Manyara

January 4, 2021

Na John Walter-Manyara

TIMU ya Soka ya Sinai Rangers imefanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi ya Mkoa wa Manyara baada ya kumaliza ligi ikiwa na alama 13.

Kila timu ilicheza mechi tano ambapo Sinai Rangers ilitoa sare moja na kushinda nne, nafasi ya pili Fighter kwa alama 11, imetoa sare moja na kushinda tatu,ya tatu Bargish ikiwa na alama 10, ametoa sare moja, kafungwa moja na kushinda tatu.

Ligi hiyo ilichezwa katika wilaya ya Mbulu.

Mwenyekiti wa mashindano Yusufu Mdoe ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya utendaji ya chama cha mpira wa miguu mkoa (MARFA) amesema ligi hiyo iliyoanza Desemba 21,2020 ilitakiwa kuwa na timu 12 lakini kutokana na ukata unaozikabili timu, 6 pekee ndizo zilizoweza kushiriki.

Amezitaja timu zilizoshiriki ni Bargish Fc, Fighter Fc, Cluster Sc, Jordom Sc,Eagle Fc na Sinai Rangers.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Abrahaman Kololi ambaye pia ni mdau wa michezo amesema atahakikisha timu hiyo inapata sapoti na kusonga mbele.

Kololi amewataka wananchi walioomba kuweka vibanda katika uwanja wa kwaraa kuharakisha ujenzi huo ili uweze kutumika katika shughuli mbalimbali pamoja na kuzialika timu za ligi kuu kuja Babati.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *