img

Naibu Waziri avunja Bodi ya Mamlaka ya Maji Rujewa kwa kushindwa kutimiza majukumu yake

January 4, 2021

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Wilaya ya Mbarali – Mbeya, kwa kushindwa kuisimamia Menejimenti ya Mamlaka hiyo kutimiza majukumu yake

Mhandisi Mahundi amechukua uamuzi huo baada ya kubaini ukosefu wa huduma ya uhakika ya maji kwa muda mrefu kwa wakazi wa Mbarali bila sababu za msingi

Pia, amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Ndele Mengo kufanya uchunguzi ndani ya siku 4 ili kubaini chanzo na kupata suluhu ya upatikanaji wa huduma ya Maji Wilayani hapo

Vilevile, amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kumuondoa Meneja wa Wilaya ya Mbarali pamoja na kufanya mabadiliko ya Wataalamu

Amesema, Wananchi wa Mbarali wana kero nyingi kuhusiana na huduma ya Maji huku wasimamizi wakishindwa kuwahudumia ila wanatoa taarifa zilizo tofauti ukilinganisha na uhalisia wa hali iliyopo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *