img

Mkoa wa mtwara waongoza ukusanyaji wa pato la Ardhi

January 4, 2021

Na Faruku Ngonyani , Mtwara.

Mkoa wa Mtwara umeshika nafasi ya kwanza kwenye ukusanyaji wa pato la ardhi kwa kukusanya 56% na kufikia malengo ya miezi 6 ya mwanzo.

Hayo yamethibitishwa na Naibu waziri wa Ardhi Nyumba maendeleo ya makazi Dk. Angelina Mabula wakati wa kikao kazi kilichowajumuisha wakurugenzi wa Halmashauri 9 pamoja na wataamu wa ardhi kutoka Mkoani Mtwara.

Dk.Mabula amewakumbusha wakurugenzi na wataalamu wa Ardhi kuhakikisha wanakusanya kodi za Ardhi ili fedha hizo ziweze kujenga miradi mbalimbali ya kimaendeleo hapa nchini.

Sambamba na hilo Naibu waziri huyo amegawa hati za nyumba 43 kwa baadhi ya wananchi waliopo Wilaya ya Mtwara na kuziagiza idara za ardhi kuhakikisha wanatoa  hati za ardhi kwa wanaohusika pindi zinapokuwa zimekamilika.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *