img

Marekani: Mamia waandamana kulalamikia ukatili wa polisi

January 4, 2021

 

Mamia ya waandamanaji wamekusanyika mjini Minneapolis kudai haki kufuatia kifo cha mwanaume mwenye umri wa miaka 23 aliyeuawa na polisi, mauaji hayo yakiwa ya kwanza kufanywa na polisi tangu mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd mwezi Mei.

Kiasi waandamanaji 1,000 walikusanyika na kuimba karibu na eneo ambalo Dolai Idd aliuawa siku ya Jumatano wakati wa jaribio la uhalifu. 

Polisi imesema Idd alikuwa anatafutwa kwa uchunguzi wa silaha.Mkuu wa polisi Medaria Arradondo ametoa video ya tukio ilioonyesha kuwa mshukiwa alifyatua risasi yake kwanza.Mauaji ya Idd, Mmarekani mwenye asili ya Kisomali yametokea kilomita chache tu kutoka sehemu ambayo polisi mzungu alimuua Mmarekani mweusi George Floyd kwa kumuwekea goti shingoni.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *