img

Maelfu ya waandamanaji Iraq wamuomboleza Soleiman mwaka mmoja baada ya kuuawa

January 4, 2021

Maelfu ya waombolezaji nchini Iraq wamesikika wakiimba nyimbo za “kisasi na “Hapana kwa Marekani” siku ya Jumapili, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya Marekani kufanya shambulio lililomuua kamanda wa jeshi la Iran Qasem Soleiman na mwenzake wa Iraq Abu Mahdi al-Muhandis.

Waandamanaji wanayoiunga mkono Iran, wengi wakivalia mavazi meusi walikusanyika katika uwanja wa Tahrir mjini Baghdad ambapo pia walimshtumu Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al Kadhemi na kumuita mwoga na kibaraka wa Marekani.

Kumbukumbu ya mashambulizi hayo ya kombora, ambayo nusra yasababishe vita kati ya Iran na Marekani mwanzoni mwa mwaka 2020, pia yaliadhimishwa nchini Iran, Syria, Lebanon, Yemen na sehemu nyengine.Iran iliandaa matukio mbalimbali ya kumbukumbu ya Soleimani mnamo siku ya Jumapili, ikimtaja kama “shahidi”.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *