img

Korti ya Uingereza yakataa ombi la Marekani la kumuhamisha Assange

January 4, 2021

 

Mahakama ya Uingereza imekataa ombi la Marekani la kumkabidhi kwake mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange ili akabiliwe na mashtaka ya ujasusi.

Mahakama imeamua kuwa hatua ya kumhamisha Assange, ni “ukandamizaji” kutokana na afya yake ya kiakili.Jaji Vanessa Baraitser amesema Assange huenda akajiua iwapo atahamishwa hadi Marekani.Hata hivyo, serikali ya Marekani imesema itakata rufaa juu ya uamuzi huo.

Waendesha mashtaka wa Marekani wanamshtumu Assange kwa makosa 17 ya ujasusi na utumizi mabaya wa Kompyuta kwa kuchapisha mtandaoni nyaraka za siri juu ya oparesheni za jeshi la Marekani nchini Iraq na Afghanistan muongo uliopita. Iwapo atapatikana na hatia, Assange huenda akapewa kifungo cha miaka 175 jela.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *