img

Kiti kinakuwa moto kwa kocha wa Chelsea Lampard

January 4, 2021

Inaonekana Arsenal imewakabidhi kijiti Chelsea au niseme Arsenal iliwaambukiza Chelsea kirusi kikali Zaidi hata Zaidi ya corona maana tangu The Gunners walipowacharaza The Blues, vijana hao wa Lampard wamekuwa katika hali mbovu wakati wenzao wa Arteta wakiendelea kuimarika. Kipigo cha cha jana cha 3 – 1 dhidi ya Manchester City kiliangamiza kabisa matumaini yoyote ya kugombea taji la ligi msimu huu.

Na Lampard anafahamu masharti ya kuwa kocha wa klabu hiyo chini ya mmliki Roman Abramovich zaidi ya mwingine yeyote maana alicheza chini ya makocha tisa tofauti katika enzi yake akiwa Stamford Bridge. Shinikizo limekuwa kali hasa kwa kuzingatia uwekezaji uliofanywa katika dirisha kubwa la usajili mwaka jana. Kuna tetesi kuwa tayari Chelsea wako sokoni kumsaka kocha mpya kama Lampard atafurushwa.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *