img

Kipanga awataka wana-Mafia kusaidia michezo

January 4, 2021

Na Omary Mngindo, Kibaha

MBUNGE wa Jimbo la Mafia Mkoa wa Pwani Omary Kipanga, amewaomba wakazi jimboni humo kusaidia kwa hali na mali sekta za michezo ili kuendeleza vipaji vya vijana.

Kipanga (Naibu Waziri wa Elimu) ametoa rai hiyo akizungumza na Waandishi wa habari mjini hapa, ambapo alisema sekta hiyo yenye wapenzi wengi inahitaji msukumo na msaada mkubwa ili kuviwezesha vipaji vilivyopo viweze kiendelea.

Alisema kuwa Mafia kuna vijana wenye uwezo mkubwa wa kushiriki michezo mbalimbali hususani soka, hivyo ni wajibu wao kuiangalia sekta hiyo kwa jicho la tatu litalosaidia kusukuma mbele zaidi vipaji hivyo.

“Serikali inahimiza michezo, hata katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inasisitiza hilo, nitumie fursa hii kuwaomba wana-Mafia hapa jimboni na nje kujitokeza kusaidia vilabu vyetu ili viweze kupiga hatua kwani ina mchango mkubwa katika ajira,” alisema Kipanga.

Akizungunzia ushiriki wa timu ya Black Rhino ya jimboni humo inayoshiriki Ligi ngazi Mkoa kuanzia hatua ya makundi mpaka sasa tisa bora, Naibu Waziri huyo alisema kuwa anaimani kwamba watafanya vizuri katika hatua hiyo, huku akiwataa wachezaji wakajitume.

“Mimi na viongozi wenzangu wa chama na serikali tumewaaga vijana wetu waliosafiri kwenda Bagamoyo kwa hatua ya tisa bora iliyoanza Jan 3 uwanja wa Mwanakalenge, imani yetu watafanya vizuri niwaombe wananchi tuwaombee dua,” alisema Kipanga.

Aidha aliwapongeza viongozi wa (FAM 97) wilayani humo kwa namna wanavyojitahidi kuusimamia na kuuendeleza, huku akionesha imani kubwa kwamba kwa kushirikiana na wadau wengine msimu ujao wa Ligi ngazi ya wilaya itakuwa bora zaidi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *