img

Fahamu jinsi umri unavyochangia mfumo wa mwili kupungua nguvu ya kupigana na magonjwa na vile unavyoweza kurekebisha hali hiyo

January 4, 2021

  • Laura Plitt
  • BBC News Mundo

Dakika 4 zilizopita

Picha ya mtu ambaye yuko katika eneo chafu huku akijaribu kujilinda dhidi ya virusi

Maelezo ya picha,

Kinga yetu hukabiliana na virusi mwilini

Mtandao wa seli, tishu na viungo vya mwili ndio silaha muhimu ya kujikinga dhidi ya maambukizi na magonjwa.

Na ndio sababu janga la virusi vya corona limeonesha umuhimu wa mfumo wetu wa kinga.

Kama sehemu nyingine yeyote ya mwili, kadiri siku zinavyokwenda, mfumo wa kinga pia nao unaendelea kuzeeka.

Hii ndio moja ya sababu- mbali na magonjwa ambayo tayari mtu yuko nayo – sababu kubwa wataalamu wanaamini watu wenye umri zaidi ya miaka 65 wako katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya corona na matatizo mengine zaidi.

Hata hivyo, kuzeeka kwa mfumo wa kinga sio kwamba kunaendana moja kwa moja na umri.

“Kunaweza kuwa na watu ambao umri wao ni miaka 80 lakini kinga yao ya mwili ni sawa na mtu mwenye umri wa miaka 62. Au hata vyinginevyo,” amesema Shai Shen-Orr, mtaalamu wa kinga katika Taasisi ya Teknolojia ya Technion Israel.

Taarifa njema ni kwamba tunaweza kupunguza mchakato wa kuzeeka kwa kufuata hatua rahisi kabisa.

Lakini kabla ya hapo, kwanza tuangalie namna mfumo wa kinga unavyofanyakazi.

madhara ya umri huathiri kinga yetu na kutuwacha tukiwa tunaweza kuambukizwa virusi vingi kama Covid 19

Maelezo ya picha,

madhara ya umri huathiri kinga yetu na kutuwacha tukiwa tunaweza kuambukizwa virusi vingi kama Covid 19

Seli zenye kupigana na magonjwa

Mfumo wa kinga una sehemu mbili kila moja ikiwa umetengenezwa kwa aina mbalimbali ya seli nyeupe za damu – ambazo zinahusika na kulinda mfumo mzima wa mwili.

Kinga ya mwili halisi ndio ya kwanza kukinga mwili. Kinga hii hufanyakazi karibu kila siku punde tu baada ya kubaini kwamba kuna viumbe vya kigeni ndani ya mwili.

Jinsi mwili unavyojibu ni pamoja na “neutrophils, inavyojulikana kwa Kiingereza ambayo hasa kuathiri bakteria; monocytes au chembe nyeupe za damu ambazo husaidia kujipanga kwa mfumo wa kinga, na kufahamisha seli zingine kwamba kuna maambukizi, na seli zingine hatari za kuua ambazo kazi yake ni kupigana na virusi ama saratani.

Tunapokuwa wazee seli hizi huwa hazifanyi kazi vizuri,” anaelezea Janet Lord, mkurugenzi wa taasisi inayoangazia kufura na kuzeeka kwa seli katika chuo kikuu cha Birmingham Uingereza.

Seli nyeupe za damu hutulinda dhidi ya viini vya maambukizi

Maelezo ya picha,

Seli nyeupe za damu hutulinda dhidi ya viini vya maambukizi

Pia kuna mfumo wa kinga unaobadilika badilika wenye chembe za limfu za T na B ambazo huwa zinapigana na aina fulani ya pathojeni yaani viini. Mabadiliko hayo huchukua siku kadhaa kabla ya kuanza lakini yakishaanza itakuwa inakumbuka viini hivyo siku za usoni na kupigana navyo tena ikiwa vitajitokeza tena.

“Unapoendelea kuzeeka, mwili hutengeneza kiwango kidogo cha limfu lakini unazihitaji katika kukabiliana na maambukizi mapya kama vile ugonjwa wa SARS-CoV-2,” anaongeza.

“Na hata zile ambazo ziliundwa na mwili wako kukabiliana na maambukizi mengine siku zilizopita huwa hazifanyikazi vizuri kadiri mtu anavyoendelea kuzeeka.”

Hiyo ni sawa na kusema kuzeeka kunasababisha kupungua kwa utendaji kazi wa mfumo wa kinga.

Thymus, ambayo uhusika na utengenezaji wa seli aina ya lymphocyte T, huanza kupungua wakati tunafikia umri wa miaka 20

Maelezo ya picha,

Thymus, ambayo uhusika na utengenezaji wa seli aina ya lymphocyte T, huanza kupungua wakati tunafikia umri wa miaka 20

Kinga ya mwili halisi inatengeneza seli za ziada lakini hizo huwa hazifanyi kazi vizuri na kinga ya mwili inayobadilika badilika na kutengeneza limfu B ambayo hutengenezwa kwenye uboho wa mfupa ndio inayotengeneza kingamwili huku limfu za T huwa zinaua viini au seli zenye maambukizi.

Kupungua kwa seli ambazo zinahifadhi kumbukumbu ya viini kunasababisha kupoteza sio tu uwezo wa kukabiliana na maambukizi lakini pia chanjo inayozuia kadiri mtu anavyoendelea kuzeeka.

Shai Shen-Orr, mtaalamu kutoka Israeli, anaelezea kuwa hiyo ndio sababu katika chanjo ya mafua “asilimia 40 ya watu wazima wenye umri wa miaka 65 na zaidi miili yao haijiweki tena katika hali ya kukpata nafuu kwa kupewa chanjo.”

Mtu akifanya mazoezi ya kukimbia

Maelezo ya picha,

Kukimbia na kufanya mazoezi ni muhimu kuimarisha kinga

Tatizo jingine ni kwamba kuzeeka kunasababisha kufura zaidi katika damu na tishu.

Mabadiliko yote hayo yanayotokea mtu akizeeka, “yanafanya iwe vigumu kupona kutokana na maambukizi au jeraha”, Encarnacion Montecino, mtafiti wa chuo kikuu cha California (UCLA), ameiambia BBC. Anasema kuwa baadhi ya maambukizi huwa sugu.

Maambukizi ambayo yalikuwa yanadhibitiwa kama vile kifua kikuu yanaweza kujitokeza tena. Na hilo linasababisha hatari ya kutokea kwa viini vipya na magonjwa kama vile saratani.

Sio kwamba kila kitu ni umri

Hata ingawa mwili unapungua nguvu kadiri siku zinavyosonga, kile kinachotofautiana ni namna kila mtu anavyopitia mchakato huo.

Mchakato huo unachangiwa na cheme za urithi, lakini pia mtindo wa maisha.

Hadi hivi karibuni haikuwa rahisi kubaini umri wa kinga ya mwili.

Lakini pia mazoezi madogo kama vile kutembea husaidia kupunguza kuzeeka kwa mfumo wa kinga mwilini

Maelezo ya picha,

Lakini pia mazoezi madogo kama vile kutembea husaidia kupunguza kuzeeka kwa mfumo wa kinga mwilini

Hata hivyo, Shen-Orr na timu yake kutoka chuo kikuu cha Stanford huko Marekani, alifanikiwa kuunda mbinu ya kupata taarifa ambazo zinaweza kuwa muhimu katika tiba.

“Kwa kuelezea aina 18 ya seli za mfumo wa king ana kuelezea chembe za mwili katika damu, tunaweza kubaini mfumo wa kinga umefika hatua gani ya kuzeeka,” anaelezea Shen-Orr.

Tofauti ni kasi ya mchakato wa kuzeeka ambako pia kunahusishwa na jinsia.

Inasemekana kuwa wanawake ambao wamefika umri wa kukoma hedhi hutengeneza homoni estrojeni ambazo zina umuhiu katika mfumo wa kinga wa wanawake.

Wataalam wanasema kwamba kukaa chini kwa muda mrefu ndio 'kuvuta sigara kupya'

Maelezo ya picha,

Wataalam wanasema kwamba kukaa chini kwa muda mrefu ndio ‘kuvuta sigara kupya’

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *