img

Drake aongoza listi ya wasanii waliosikilizwa zaidi 2020

January 4, 2021

 

Mwaka 2020 ulikua na changamoto nyingi karibu katika kila sekta lakini haijazuia dunia ya kidigitali kufanya maajabu, tumezishuhudia listi za wasanii kwenye chat mbalimbali za mitandao ya ku-stream muziki kama Soundcloud, Apple Music na hata pia Spotify kwa kuongoza kusikilizwa zaidi.

Vipi ikawepo listi inayojumuisha wasanii kutoka kwenye chat za mitandao yote hiyo na ikafahamika wasanii gani wamesikilizwa zaidi 2020?

Mwishoni mwa wikiendi iliyoisha, mtandao wa HITS Daily Double, umetoa list ya wasanii vinara 50 wa kusikilizwa kwenye mitandao yote ya ku-stream muziki kwa mwaka 2020, ambapo rapa Drake ameongoza kwenye listi hiyo kwa kusikilizwa mara zaidi ya Bilioni 5.6 kwenye mitandao yote.

Kwenye orodha hiyo namba mbili inashikiliwa na Juice WRLD ambaye amesikilizwa mara zaidi ya Bilioni 5.3, Young Boy kashika namba tatu akiwa amesikizwa zaidi ya mara Bilioni 4.6. Namba nne inashikiliwa na Lil Uzi Vert akiwa na 3.9 na namba tano inashikiliwa na Post Malone akiwa na 3.7.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *