img

China yaikosoa Marekani kwa kuingiza siasa kwenye biashara

January 4, 2021

 China imesema inapinga tabia ya Marekani ya kuingiza siasa katika masuala ya biashara baada ya soko la hisa la New York kuanza kuondoa kampuni tatu za mawasiliano za China.

Marekani imesema kampuni hizo za China zina uhusiano na jeshi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Hua Chunying, ameuambia mkutano wa waandishi habari kuwa China itachukua hatua zinazohitajika ili kulinda haki za kisheria za kampuni zake.

Wiki iliyopita, soko la hisa la New York lilianza kuziondoa kampuni za China: China Mobile, China Unicom na China Telecom baada ya uamuzi wa Rais Donald Trump kuzuia uwekezaji wa Marekani katika kampuni zinazomilikiwa na jeshi la China.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *