img

Bilionea Jack Ma hajulikani alipo

January 4, 2021

Uvumi umezagaa kuhusu wapi alipo Bilionea wa China, Jack Ma kutokana na kutojitokeza kwake hadharani kwa muda wa miezi miwili.

Jack Ma ambaye ni mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba hajaonekana katika sehemu ya mwisho ya kipindi chake alichokianzisha cha ‘Africa’s Business Heroes,’ kinachowapa fursa wafanyabiashara wanaochipukia katika Bara la Afrika.

Ma alitakiwa kuwa miongoni mwa majaji katika fainali hiyo lakini nafasi hiyo ikachukuliwa na mmoja wa viongozi wa juu wa kampuni yake ya Alibaba na picha yake ikaondolewa katika tovuti kama atakuwa miongoni mwa majaji wa fainali hizo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Financial Times ulimnukuu Msemaji wa kampuni hiyo akisema kuwa Ma hakuweza kutokea katika tukio hilo kutokana na mgongano wa ratiba jambo lililozua minong’ono duniani kote watu kutaka kujua bilionea huyo yupo wapi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *