img

Ujerumani huenda ikarefusha hatua za kuzuia kusambaa COVID-19

January 3, 2021

 

Kutokana na hali ya kuongezeka kwa vifo na maambukizi ya virusi vya corona nchini Ujerumani, inaelekea kutakuwapo na makubaliano kwenye majimbo yote 16 juu ya kurefusha muda wa kutekeleza hatua kali za kuzuia kuenea kwa maambukizi. 

Muda wa hapo awali ulikuwa hadi tarahe 10 mwezi huu. Uamuzi utatolewa Jumanne ijayo kwenye mkutano kati ya mawaziri wakuu wa majimbo yote 16 na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel. 

Taasisi ya Ujerumani ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza ya Robert Koch imesema watu wapatao 16,718 walikufa kati ya mwezi Desemba hadi Januari mosi. Idadi ya walioambukizwa ilifikia 1,719,737 hadi mwezi uliopita. Madaktari wametoa mwito wa kuchukuliwa hatua kali zaidi ili kupunguza maambukizi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *