img

DRC yawasamehe wanaume waliomuua rais Laurent Kabila

January 3, 2021

 

Wanaume wawili waliopatikana na hatia ya mauaji ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Laurent Kabila miaka 20 iliyopita wamepewa msamaha.

Japo Bw. Kabila alipigwa risasi na mlinzi wake, maafisa wake wawili wa ngazi ya juu, Kanali Eddy Kapend na Georges Leta, walihusishwa na mauaji hayo.

Rais Félix Tshisekedi ilibadilisha hukumu ya kifo dhidi yao mwezi Juni mwaka uliyopita.

Hatua hiyo inajiri wakati kuna mvutano kati ya Rais Félix Tshisekedi na mtangulizi wake, Joseph Kabila ambaye ni mwana wa kiume wa Laurent Kabila.

Joseph Kabila alichukua madaraka baada ya kifo cha baba yake mnamo 2001 na alitawala DR Congo kwa miaka 18 kabla ya Bw Tshisekedi kushinda uchaguzi mnamo Desemba 2018.

Ingawa ulikuwa upokezanaji wa madaraka wa kwanza wa amani nchini humo kwa karibu miaka 60, wengi walipinga matokeo ya uchaguzi.

Kumekuwa na tuhuma kali kwamba rais huyo mpya alifanya makubaliano ya nyuma ya pazia na Joseph Kabila, ambaye bado ana ushawishi mkubwa nchini.

Ofisi ya Rais Tshisekedi ilisema msamaha wa rais ulitolewa kwa kila mtu aliyehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani na ambao walikuwa wametumikia vifungo vyao kufikia tarehe 31 Desemba.

Giscard Kusema, wa ofisi ya habari ya rais, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba Kanali Kapend na watuhumiwa wenzake “wananufaika na msamaha wa urais …. ambayo ni kipimo cha upeo wa jumla na tabia isiyo ya kibinadamu”.

Col Kapend alikuwa mtumishi wa karibu wa Laurent Kabila. Alipatikana na hatia ya kupanga mauaji, pamoja na maafisa wengine kadhaa wa kitngo cha usalama cha marehemu rais, pamoja na mkuu wa upelelezi wa wakati huo Georges Leta. Wote wawili walipinga kuhusika na njama hiyo.

Msamaha huo wa rais imetolewa wiki chache baada ya Rais Tshisekedi kuvunga muungano wake na chama cha Kabila – kilicho na wabunge wengi – baada ya kuongezeka kwa taharuki.

Rais kwa sasa anatafuta washirika wampya watakaoungana naye ili apate kuwa na wabunge wengi ndani ya bunge.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *