img

Waziri Jafo afurahishwa na kuipongeza halmashauri ya manispaa ya Lindi

December 15, 2020

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo amefurahishwa na kuipongeza halmashauri ya manispaa ya Lindi kwa matumizi mazuri ya fedha za umma zilizotumika kukarabati shule ya sekondari ya Lindi na ujenzi wa machinjio ya kisasa.

Waziri Jafo ametoa pongezi hizo leo kwa nyakati na maeneo tofauti alipotembelea shule ya sekondari ya Lindi iliyopo mjini Lindi na machinjio ya kisasa katika mtaa wa Ngongo, manispaa ya Lindi.

Waziri Jafo alisema serikali imetenga fedha na kupeleka katika katika shule za kihistoria ili zitumike kwa ukarabati wa shule hizo. Kwahiyo ziara yake imelenga kujiridhisha  kama fedha hizo zinatumika kama ilivyotarajiwa.

Alisema ameridhishwa na matumizi ya fedha zilizotumika kukarabati shule ya sekondari ya Lindi. Kwani hata majengo yaliyo ungua moto yameanza kurudi katika hali yake ya awali. Lakini pia kazi zilizofanyika ni nyingi kuliko ilivyotarajiwa.

Alibainisha kwamba baadhi ya kazi hazikuwa kwenye mpango. Hata hivyo zimefanyika kwakutumia fedha zilizopelekwa. Huku kazi zote zilizopangwa zifanyike kwakutumia fedha hizo zimefanyika. Kitendo ambacho nichakupongezwa na kupigiwa mfano.

Kuhusu majengo yaliyoungua moto, waziri Jafo aliahidi kutuma wataalamu wataokwenda kufanya tathimini ili kujua mahitaji na gharama ya kukarabati. Nia ikiwa ni kurejesha hali ya shule hiyo katika sura ya awali kama ilivyokuwa kabla ya kuungua moto.

Aidha kwa upande wa machinjio ya kisasa ambayo ujenzi wake ukikamilika itakuwa ni miongoni kwa vyanzo vikubwa vya mapato kwa halmashauri ya manispaa ya Lindi, Waziri Jafo alisema ameridhishwa na kufurahishwa na hatua iliyofikia katika ujenzi huo.

Alisema licha ya kupigwa hatua kubwa ya ujenzi, lakini pia ujenzi huo unazingatia viwango. Hali ambayo imesababisha machinjio hayo kuwa ni miongoni mwa machinjio bora.Huku akibanisha kwamba matumizi ya fedha yamelingana na kazi iliyofanyika.

” Mheshimiwa mkuu wa mkoa nimefurahi naniwapongeza, hapa wala sina maneno. Mradi huu nimetembelea mara nyingi, mwanzo nilipata mashaka na kasi ya ujenzi. Lakini kwa kasi ya sasa na hatua iliyofikiwa nawapongeza,” alisema mheshimiwa Jafo.

Waziri huyo mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa ambae aliutaja mradi huo kama mtaji anzia wa halmashauri hiyo  alisema mradi huo utawekwa kwenye mpango miongoni mwa miradi ya kimkakati ili uweze kumalizika na kutoa huduma.

Alisema anakila sababu ya kufanya hivyo, kwani anatambua kwamba Lindi haina mradi mkakati. Kwahiyo kuna haja ya kuongeza nguvu ili ukamilikeharaka.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Lindi, Jomaary Satura alisema katika halmashauri ya manispaa ya Lindi kuna ng’ombe wengi. Hivyo mradi huo ukikamilika utakuwa ni miongoni mwa vyanzo vya mapato vinavyoingiza fedha nyingi kwa halmashauri hiyo.

Kabla ya kutembelea shule ya sekondari ya Lindi na machinjio ya kisasa, waziri Jafo alitembelea shule ya Kilangala iliyopo katika kata ya Kitomanga, jimbo la Mchinga ambako pia alifurahishwa na ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule hiyo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *