img

Watu 3 wafariki kwenye baada ya meli mbili kugongana nchini China

December 15, 2020

 Watu 3 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na ajali ya meli mbili zilizogongana katika Mto Yangzi unaopita mji wa Shanghai nchini China.

Meli hizo mbili za makontena zinazoitwa “Oceana” na “Xinqisheng 69”, ziligongana katika eneo ambalo mto unatiririkia kwenye Bahari ya Mashariki ya China.

Kwa mujibu wa taarifa za China Daily, meli ya Xinqisheng 69, yenye urefu wa mita 165 na iliyokuwa imebeba makontena 650, ilipinduka baada ya ajali hiyo ya mgongano.

Timu ya uokoaji iliwawaokoa wafanyakazi 8 kati ya 16 waliokuwemo kwenye meli, na kupata maiti za watu 3.

Shughuli ya utafutaji wa watu wengine 5 waliopotea bado inaendelea.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *