img

Wana-UVCCM wanne wasimamishwa Mkuranga

December 15, 2020

Na Omary Mngindo, Kibaha Des 15

WANACHAMA wanne wa Jumuia ya Vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, wamesimamishwa uongozi na Baraza Kuu la Jumuia hiyo.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na Baraza hilo imetokana na wanachama hao wanne kuongoza Maandamano ya kutomtaka Katibu wa Jumuia wilaya Hanzuruni Mtebwa, kitendo ambacho ni kinyume cha kanuni ya UVCCM.

Aliwataka waliosimamishwa huku wakikatazwa kujihusisha na shughuli za Jumuia kuwa ni Omari Mataka Mwenyekiti wa Kata, Abdallah Nunda Katibu Rehema Kiuta Katibu wa hamasa Kata na Mosi Siri wote kutoka wilayani humo.

Akizungumza na Wajumbe wa Kikao chini ya Mwenyekiti wa Baraza la UVCCM Samaha Said, alisema kuwa Jumuiya hiyo haitowafumbia macho wanachama wenye nia ya kutaka kuwavuruga, na kwamba hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa wote wataobainika.

Alisema kuwa moja ya sababu zilizosababisha kuwasimamisha,

 imetokana na maamuzi mabaya waliyoyachukua dhidi ya katibu wao, huku wakijua fika kanuni za Jumuiya zinavyose.a kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo Jumuia hiyo.

“Tumewasimamisha uongozi viongozi hao kutokana na utovu wa nidhamu wa hali ya juu waliouonyesha, wamekuwa wakitumika vibaya na baadhi ya viongozi wanaohitaji madaraka, tukiwa viongozi wa Jumuia tumeamua kuwasimamisha uongozi,” alisema Samaha.

Kwa Upande wake Mjumbe wa Baraza kuu Taifa kutokea Mkoa wa Pwani Ramadhani Mlao, amebariki uamuzi huo na kwamba hatua hiyo itendelea kuchukuliwa kwa vijana wataobainika kujihusisha na vitendo kama hivyo, huku akitoa onyo kwa wana-UVCCM.

Aliongeza kuwa Jumuia ina nguvu kuliko mtu yeyote, hivyo kwa vijana waliosimamishwa uongozi ni fundisho kubwa kwa kiongozi yeyote anayejiona kujiona ana nguvu kuliko Jumuia, kitendo ambacho hakikubaliki. 

Aidha Mlao ametoa ushauri kwa vijana kuwa, wakati wa sasa ni wa vijana kujitambua na kuacha tabia ya kutumikishwa kama punda, hivyo kila mmoja ajitafutie kipato chake binafsi ili kuondokana na tabia zinazofanywa na watu wenye madaraka.

Naye Pendo Moreto Katibu wa Hamasa kutokea Wilaya ya Bagamoyo pia Mjumbe wa Baraza hilo, alipongeza hatua hiyo huku akieleza kuwa Jumuia hiyo ni chombo kinachowaandaa vijana kushila nyadhifa mbalimbali ndani ya chama na Serikali hivyo haitawafumbia macho wanaotaka kukiharibu.

Alisema kuwa anajisikia aibu kubwa kwa vijana wenzao kuona wakipewa barua za kusimamishwa uongozi ndani ya Jumuia, lakini ndio kanuni zao ambapo  kila mmoja wetu anazitambua.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *