img

Wajumbe wathibitisha ushindi wa Biden

December 15, 2020

Wajumbe wakiwa wamepiga kura siku ya Jumatatu, walimpa rasmi Joe Biden zaidi ya kura 270 za uchaguzi zinazohitajika kuthibitisha ushindi wake wa uchaguzi.

Pamoja na kura 55 za wajumbe kutoka California, kati ya za mwisho kupigwa Jumatatu, Biden ana kura 302 za uchaguzi, zaidi ya kiwango kinachohitajika kushinda urais.

Biden amekuwapo kwenye uwanja wa siasa za Marekani kwa karibu nusu karne, na ushindi wake katika kura za wajumbe umemfanya Trump, Mrepublican, rais wa tano wa Marekani katika historia ya miaka 244 ya nchi hii kupoteza uchaguzi baada ya muhula mmoja katika Ikulu ya Marekani.

Kura ya wajumbe ni ya uthibitisho wa utaratibu wa kawaida kwenye kalenda ya uchaguzi wa urais wa Marekani. Lakini tangu kura ya kitaifa ya Novemba 3, Trump amedai mara kwa mara bila ushahidi wwowote wa kuaminika kwamba kura katika majimbo yaliokuwa na ushindani mkali aliyopoteza kwa Biden kwa viwango tofauti ilikuwa ya wizi ikimgharimu kuchaguliwa tena.

Trump na washirika wake wamepoteza kesi zaidi ya 50 katika majimbo yenye ushindani mkali wanakopinga matokeo ya kura hiyo.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA ,Washington DC

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *