img

Ujerumani yashinikiza Umoja wa Ulaya kuidhinisha chanjo ya COVID-19

December 15, 2020

 

Ripoti inaeleza kwamba Ujerumani inaushinikiza Umoja wa Ulaya kuongeza kasi ya kuidhinisha matumizi ya chanjo ya virusi vya corona wakati huu ikipambana na ongezeko la maambukizi. 

Msukumo huo unatolewa katika katika kipindi ambacho Marekani na Uingereza zikiwa tayari zimeanza jitihada za utekelezaji wa chanjo kwa umma. 

Likinukuu chanjo, ambacho hakikutajwa kwa jina, gazeti la leo la Bild la Ujerumani limeandika ofisi ya Angela Merkel na Wizara ya Afya ya Ujerumani zinataka Wakala wa Afya wa Ulaya (EMA) kuifanya Desemba 23 hadi 29 kuwa ni muda wa chanjo ya makampuni ya Pfizer na BioNTech. 

Ujerumani inajiandaa kuingia katika kufungwa kwa shughuli za umma kwa wastani kuanzia kesho Jumatano, ambapo maduka yasio yalazima yatafungwa na shule pia kufungwa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *