img

Somalia yakatiza uhusiano wa kiplomasia na Kenya

December 15, 2020

Viongozi wa Somalia na Kenya washawahi kufanya mazungumzo ya kusuluhisha mzozo kati ya nchi hizo mbiliImage caption: Viongozi wa Somalia na Kenya washawahi kufanya mazungumzo ya kusuluhisha mzozo kati ya nchi hizo mbili

Serikali ya Somalia imekatiza uhusiano wa kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya.

Nchi hiyo imewaita nyumbani wanadiplomasia wake wote kutoka Nairobi na kuwapatia wanadiplomasia wa Kenya muda wa siku saba kuondoka nchini humo.

Tangazo hilo limetolewa na Waziri wa Habari Osman Abukar Dubbe katika chombo cha habari cha kitaifa.

“Serikali ya Somali, kulingana uhuru wake iliyohakikishiwa na sheria ya kimataifa, inatekeleza wajibu kwa mujibu wa katiba ili kulinda utaifa, umoja na ustawi wa nchi imeamua kukatiza uhusiano wake wa kidiplomasia na serikali ya Kenya,” alisema.

Hatua hiyo inakuja baada ya Somalia kuwasilisha barua ya malalamiko dhidi ya Kenya kwa Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Viongozi wa nchi wanachama wa muungano wa maendeleo Afrika Mashariki na pembe ya Afrika (IGAD).

Hivi karibuni Somalia iliituhumu Kenya kwa kuingilia masuala yao ndani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *