img

Shambulio la shule Nigeria: ‘Jinsi nilivyotoroka watekaji’

December 15, 2020

Dakika 6 zilizopita

school boys in uniform

Mwanafunzi aliyefanikiwa kutoroka baada ya majambazi waliokuwa wamejihami kwa silaha kuvamia shule ya bweni ya wavulana nchini Nigeria amezungumza na BBC

Mwanafunzi huyo aliye na umri wa miaka 17-(ambaye jina lake tumelibana ) alitekwa pamoja na wenzake zaidi ya 500 kutoka shule ya upili ya sayansi ya serikali kaskazini-magharibi mwa jimbo la Katsina usiku wa Ijumaa .

“Tulikuwa tukisukumwa na kupigwa, tulitembea usiku kucha, wakati mwingine kwenye miba. dakika thalathini kabla ya alfajiri tuliambiwa tulale,” aliambia BBC Hausa.

Alisema wakati wenzake walikuwa wanapumzika, alipata nafasi y akujificha.

“Nilikaa chini ya mti, na kuegemea mti huo kidogo, hadi nilipopata sehemu nzuri ya kujificha. Nililala chini na kunyoosha miguu yangu.”

Wakati majambazi hao walipowaamuru wanafunzi wenzangu kuanza tena safari, hawakugundua nilikuwa nimejificha nyuma ya mti

“Baada ya kila mtu kuondoka, Nilianza kutafuta njia salama ya kutoka, hadi nikafika kijiji kilichokuwa karibu, kwa kweli ni kwa neema ya Mungu nilifanikiwa kutoroka,” alisema.

Map

Gavana wa jimbo la Katsina Aminu Bello Masari amesema wanafunzi 333 bado hawajulikani waliko lakini haijabainika ni wangapi waliotekwa, kwani baadhi yao huenda wametoroka na wengine hawajapatikana. Pia amesem awatekaji hao wamewasiliana na kwamba mashauriano yanaendelea.

Hata hivyo msemaji wa Rais wa Nigeria Garba Shehu, alikuwa ameambia BBCkwamba watoto waliotoroka ni 10 huku wenzao wakisalia na majambazi waliojihami kwa bunduki.

Walisema wao ni maafisa wa usalama

Mwanafunzi aliyefanikiwa kutoroka alisema wanaume hao waliyokuwa wamejihami waliingia katika shule yao karibu saa tatu usiku (20:30 GMT) Ijumaa na kuongeza kuwa wanafunzi wengi waruka ua la shule waliposikia milio ya risasi.

Hata hivyo walipatikana na majambazi walikuwa na tochi waliowahadaa kuwa maafisa wao usalama na kuwaomba warudi shuleni.

Wanafuzi walijua baadae kuwa wanaume hao sio maafisa wa usalama kama walivyowaambia.

School sign

Maelezo ya picha,

Shule hiyo iko eneo la vijijini kaskazini -magharibi mwa Nigeria

Wakati huo inaaminiwa ndio majambazi hao waliwakusanya pamoja wanafunzi na kuwalazimisha kutembea na kuingia msitu ulioko karibu.

“Baada ya kuingi msituni, mmoja wao alituamuru tusimamame na ambapo tulihesabiwa kabla ya kuendelea na safari,” alisema.

Alisema kuwa wanafunzi 520 walihesabiwa na kwamba hakuona hat ammoja wao alipotoroka.

Serikali imelaumu majambazi ambao huwateka watu na kuitisha kikombozi kwa kuhusika na shambulio hilo

Majambazi hao ni kina nani?

Katika eneo la kaskazini -magharibi mwa Nigeria, neno “majambazi” linatumiwa kuashiria wafugaji wa jamii ya Fulani, makundi ya kutoa ulinzi yaliyojihami na hata wanamgambo wa Kiislamu wanaotoroka mashambulio katika eneo la kaskazini -mashariki.

Baadhi ya viongozi wa makundi hayo ya majambazi, ambayo yanajihusisha na utekaji nyara na kushambulia jamii ya wakulima, washawahi kukutana hadharani na magavana na viongongozi wengine wa serikali wakati wa mzungumzo ya kutafuta amani yaliyotibuka.

Lakini hiii ni mara ya kwanza majambazi hao wamewateka wanafunzi kutoka shuleni – mbinu ambayo ilitumiwa na makundi ya zamani kama vile Boko Haram na swap, hali ambayo imezua hofu kwamba makundi hayo ya uhalifu kaskazini -magharibi mwa Nigeria sasa yanaiga wanamgambo wa Kiislamu.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *