img

Sababu za Mama kuamua kumuuza mwanae Kenya kwa pauni 70

December 15, 2020

  • Na Joel Gunter
  • BBC Africa Eye

14 Disemba 2020

Adama akiwa na mtoto wake aliyetakiwa kumuuza
BBC

Mwezi uliopita, BBC Africa Eye kufichua biashara haramu ya watoto katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Polisi waliwakamata watu saba kwa makoa ya kusafirisha watu. lakini vipi kuhusu wanawake wa upande mwingine wa mikataba hii haramu? Ni nini kinachomsukuma mama kuuza mtoto wake kwa pauni 70?

BBC

Maisha ya Adama yalikuwa rahisi wakati alipokuwa na wazazi wake, alisema. Pesa ilikuwa ngumu, na hakuwa na uchaguzi, lakini kulikuwa na agizo kwa vitu ambavyo vilikuwa na maana. Alihudhuria shule na aliipenda sana. Alikuwa na wasiwasi kiasi. Halafu baba yake alifariki akiwa na miaka 12, na mama yake alifuata miaka michache baadaye.

“Maisha yalikuwa magumu wakati huo,” alisema, katika mazungumzo kutoka katika kijiji chake huko Mashariki mwa Kenya. “Nililazimika kuacha shule na kujitunza mwenyewe.”

Akiwa na miaka 22, Adama alikutana na mwanaume na akapata ujauzito, lakini alifariki siku tatu baada ya mtoto wao wa kike kuzaliwa. Upweke wake uliongezeka. Alimnyonyesha mtoto wake kwa ugonjwa wa watoto wachanga hadi alipopona, takriban miezi 18, kisha kipato cha kutosha kilihitajika kuwafanya wote wawili waweze kuishi. Hivyo Adama alimwacha mtoto na bibi yake mzee na kuelekea Nairobi kutafuta kazi.

“Kumbuka kuwa unakwenda kupata riziki kwa ajili ya mtoto wako,” Bibi yake alisema.

BBC
BBC

Adama alifika Nairobi na kuanza kwa kuuza Matikiti maji barabarani, lakini haimkulipa vya kutosha na mwenzake aliyeishi naye nyumbani aliiba pesa yote aliyoiacha ndani. Maisha katika jiji yalikuwa magumu pia: ana kovu kwenye paji la uso wake, chini ya nywele zake zilizokatwa, kutokana na kujitetea. “Wanaume wengine walikuwa wakinikorofisha na ilifikia hatua ilibidi nipigane,” alisema.

Aliendelea kufanya kazi ya ujenzi, ambapo hakulipwa kabisa, na kutoka hapo alikwenda kwenye kilabu cha usiku, ambapo alimuagiza bosi wake ampe moja kwa moja fedha bibi yake kijijini. Baada ya muda, Adama alichukua mshahara kidogo huko Nairobi ili aweze kupanga mahali pa kuishi. Alipata kazi mpya na mshahara bora kidogo kwenye eneo jingine la ujenzi, na alikutana na mwanaume huko. Wawili hao walichumbiana kwa muda na akamwambia anataka kupata mtoto.

Adama alimpa sharti – ikiwa angeweza kumleta mtoto wake wa kike kuishi nao, wangeweza kupata mtoto pamoja. Alikubali, na kwa miezi mitano ya ujauzito wa Adama alilipa kodi na bili na alinunua chakula kwa ajili ya nyumba yao, na Adama alisubiri wakati mzuri wa kumleta mtoto wake mjini. Kisha akaondoka siku moja na hakurudi tena.

BBC
Maelfu ya wasichana hupata ujauzito kila mwaka nchini Kenya

BBC

Wanawake wengi watajua wasiwasi wa kujiandaa kumleta mtoto ulimwenguni bila pesa ya kutosha kulisha mtu mmoja, achilia mbali wawili. Wengi hawatawahi kufikiria kuuza mtoto kwa mgeni. Lakini kwa akina mama wengine wajawazito katika umasikini nchini Kenya, kuuza mtoto kwa wafanyabiashara imekuwa wazo la mwisho ili kuweza kuishi.

Wafanyabiashara hao hulipa kiasi kidogo cha kushangaza. Sarah alikuwa na umri wa miaka 17 wakati alipopata ujauzito kwa mtoto wake wa pili, bila kuwa na namna ya kumsaidia mtoto huyo, alisema. Alimuuza kwa mwanamke ambaye alimpa shilingi 3,000 za Kenya – karibu pauni 20.

“Wakati huo nilikuwa mdog, sikuwahi kufikiria kile nilichokuwa nikifanya kilikuwa kibaya,” alisema. “Baada ya miaka mitano iliniumiza, na nilitaka kumrudishia pesa.”

Alisema anajua wanawake wengine ambao walikuwa wamewauza watoto wachanga kwa pesa kama hiyo.

“Wasichana wengi huuza watoto wao kwa sababu ya changamoto. Labda amefukuzwa nyumbani na mama yake na hana kitu, au alikuwa bado shuleni wakati alipopata ujauzito. hii ni shida nyingi kwa msichana ambaye ana miaka 15 au 16.

“Utakuta wasichana wanapoteza watoto wao na kila kitu wanachomiliki kwa sababu hakuna mtu wa kuwashika mkono.”

BBC
Adama hakuambiwa chochote kuhusu kuasili mtoto kisheria

Kenya ina moja ya viwango vya juu zaidi vya mimba zaa utotoni barani Afrika, na wataalam wa afya wanasema hali imekuwa mbaya wakati wa janga la virusi vya corona, na wanawake wengine wanasukumwa kufanya kazi ya ngono ili kuishi na wasichana kupoteza muundo wa mfumo wa shule.

“Nimesikia hadithi nyingi za wanawake na wasichana katika hali hii. Mabinti huja katika miji kutafuta kazi, kuingia katika mahusiano, kushika mimba, na kutelekezwa na baba wa mtoto,” alisema Prudence Mutiso, mwanasheria wa haki za binadamu ambaye ni mtaalamu wa masuala ya ulinzi wa mtoto na haki za uzazi.

“Ikiwa baba hatalipa, basi wanawake na wasichana hawa wanapaswa kutafuta njia zingine za kubadilisha mapato hayo. Na hiyo ndiyo inayowachochea kwenda kwa kwa wauzaji hawa wa watoto, ili waweze kupata kipato cha kujikimu na labda watoto walio nao nyumbani. Watu hawazungumzii hili kwa uwazi, lakini hili lipo.

Adama alificha ujauzito wake kwa muda mrefu kadiri alivyoweza, kwenye eneo la ujenzi, hadi ilipofikia hali ya kushindwa kubeba tena mifuko mizito ya saruji au kujificha tumbo lake. Halafu hakuwa na mapato ya kulipia kodi yake. Kwa miezi mitatu, mwenye nyumba alimpa neema, kisha akamfukuza.

Katika ujauzito wa miezi minane, Adama alianza kuvunja nyumba usiku sana ili kulala tu na kuondoka mara kunapokucha asubihi.

“Siku nzuri ningebahatika kupata chakula,” alisema. “Wakati mwingine nilikuwa nikinywa maji tu, kusali, na kulala.”

BBC
Kenya imeshuhudia ongezeko la mimba za utotoni katika miaka ya karibuni

Wakati mwanamke anajikuta katika nafasi ya Adama nchini Kenya, sababu kadhaa zinaweza kuwasukuma mikononi mwa wafanyabiashara. Utoaji mimba ni haramu isipokuwa maisha ya mama au mtoto yapo hatarini, ikiacha njia mbadala tu zisizokubalika . Kuna pia ukosefu mkubwa wa elimu ya ngono na afya ya uzazi kwa vijana, haswa vijijini, na vile vile ukosefu wa ufahamu juu ya michakato ya kisheria ya kuasili watoto.

“Wanawake na wasichana walio na mimba zisizohitajika hawana msaada kutoka kwa serikali,” alisema Ibrahim Ali, mratibu wa Kenya kwa shirika la misaada la Afya . “Wanawake hawa mara nyingi wamekuwa wakiteswa na kunyanyapaliwa, haswa katika maeneo ya vijijini, na huwa wanakimbia, na hiyo inawaweka katika mazingira magumu mijini.”

Adama hakujua ni chaguo gani la kisheria ambalo lingekuwa wazi kwake kumtoa mtoto wake salama, na hakuelewa mchakato wa kuasili. “Sikujua kabisa,” alisema. “Sikuwahi kusikia habari zake.”

Alifikiria utoaji wa mimba, alisema, lakini hakukubaliana na wazo hilo na imani yake. Kisha akafikiria kujitoa uhai.

“Nilikuwa na msongo wa mawazo, nilianza kufikiria ni jinsi gani ningejiua kwa kuzama kwenye maji , kwa hivyo watu wangenisahau tu.”

Lakini wiki chache kabla ya kujifungua, mtu mmoja alimtambulisha Adama kwa mwanamke aliyevaa vizuri anayeitwa Mary Auma, ambaye alimwambia asitoe mimba au kuukatisha uhai wake. Mary Auma anaendesha kliniki ya barabarani kinyume cha sheria katika makazi duni ya Nairobi Kayole. Alimpatia Adamu shilingi 100 na kumwambia aende kliniki siku iliyofuata.

BBC
Mary Auma

Kliniki ya muda mfupi ya Mary Auma sio kliniki, ni vyumba viwili vilivyofichwa nyuma ya duka la mbele kwenye barabara ya Kayole. Ndani kuna rafu chache tupu zilizotawanyika na bidhaa za zamani za dawa, nyuma yake kuna vyumba vya wanawake kujifungulia. Auma anakaa ndani na msaidizi wake, akinunua na kuuza watoto kwa faida, bila usumbufu wa kufuatiliwa kuhusu ni nani ananunua au nini.

Alimwambia Adama kuwa wanunuzi wake walikuwa wazazi wenye upendo ambao hawawezi kushika mimba, ambao watamtunza mtoto anayetafutwa sana. Auma huwaambia akina mama watarajiwa kuwa yeye ni muuguzi wa zamani, lakini hana vifaa vya matibabu, ustadi, au usafi wa mazingira kushughulikia shida kubwa wakati wa kujifungua. “Mahali pake palikuwa pachafu, alitumia mkebe mdogo kwa ajili ya damu, hakuwa na beseni, na kitanda hakikuwa kisafi,” Adama alikumbuka. “Lakini nilikuwa nimekata tamaa, sikuwa na la kufanya.”

Wakati Adama alipofika kliniki, Mary Auma alimpa vidonge viwili bila onyo, ili kuongeza uchungu, Adama alisema. Auma alikuwa na mnunuzi aliyepangwa na alikuwa na shauku ya kuuza. Lakini wakati Adama alijifungua, mtoto wa kiume alipata shida ya kifua na alihitaji utunzaji wa haraka, na Auma akamwambia Adama ampeleke hospitalini.

Baada ya wiki moja hospitalini, Adama aliruhusiwa na mtoto wa kiume mwenye afya. Mmiliki wa nyumba ambaye alikuwa amemfukuza wakati alikuwa mjamzito alimruhusu kurudi na alimnyonyesha mtoto. Muda mfupi baada ya kumkimbilia Mary Auma tena , alisema, na Auma akampa shilingi nyingine 100 na kumwambia aende kliniki siku inayofuata.

“Kifurushi kipya kimezaliwa,” Auma alimtumia meseji mnunuzi wake. “Shilingi 45,000 za Kenya.”

BBC
Adama

Mary Auma hakuwa akimpa Adama shilingi 45,000 – Pauni 300 – . Alimpa Adama 10,000 – karibu pauni 70. Lakini Mary Auma hakujua mnunuzi ambaye alikuwa amejipanga alikuwa mwandishi wa siri anayefanya kazi na BBC, kama sehemu ya uchunguzi wa mwaka mzima kuhusu ulanguzi wa watoto.

Wakati Adama alipokwenda kliniki siku iliyofuata, alikaa kwenye chumba cha nyuma, akimbembeleza mtoto wake mchanga mikononi mwake. Katika mazungumzo ya kunong’ona, anayedhaniwa kuwa alimwambia alikuwa na chaguzi zingine, na Adama alibadili mawazo . Aliondoka kliniki siku hiyo akiwa amemshikilia mtoto wake, na kumpeleka kwenye nyumba ya kutunza watoto inayoendeshwa na serikali, ambapo angetunzwa hadi hapo mpango w kuasili watoto utakapotimia. BBC ilimtaka Mary Auma kujibu kuhusu madai hayo katika simulizi hii, lakini alikataa.

Adama ana miaka 29 sasa, na anaishi tena katika kijiji alicholelewa. Bado hulala na njaa wakati mwingine. Maisha bado ni magumu. Anapata kazi mara kwa mara katika hoteli ndogo ya karibu lakini haitoshi. Anajitahidi kutokunywa. Ana ndoto ya kufungua duka lake la viatu kijijini na kupeleka viatu kutoka Nairobi, lakini ni ndoto ya mbali. Hawana mawasiliano na mtoto wake, lakini hajuti.

“Sikufurahi kuuza mtoto wangu, sikutaka hata kugusa pesa hizo,” alisema. “Wakati hakukuwa na pesa iliyohusika katika kumtoa, basi nilikuwa sawa.”

Anajua nyumba ya watoto mahali ambapo alimwacha mtoto wake. Ni karibu na nyumba aliyofukuzwa wakati alikuwa karibu kumzaa. “Najua eneo hilo liko salama,” alisema, “na watu wanaomtunza ni wazuri.”

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *