img

Mtoto wa pili wa Obama “Sasha Obama” na mambo mengine matatu kumuhusu

December 15, 2020

Dakika 5 zilizopita

Sasha Obama

Sasha Obama imeibua hisia mbali mbali katika mitandao ya kijamii baada ya watu kuona picha yake akiwa katika mojawapo ya sherehe na picha hii ikaanza kusambazwa kwenye mitandao hiyo.

Akiwa ni binti wa pili wa rais mweusi wa kwanza wa Marekani Barak Obama , Sasha hafahamiki sana kwa kuwa hajajisajiri kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini huonekana mara kadhaa katika mitandao ya kijamii.

Wiki iliyopita alisababisha gumzo kubwa mitandaoni , baada ya kuonekana kwa video yake akidensi na vijana wenzake katika mtandao wa Tiktok.

Haya ndio baadhi ya mambo ambayo huenda ungependa kuyafahamu kumuhusu Bi Sasha Obama ambaye sasa ana umri wa miaka 19.

Sasha Obama

Anasoma katika Chuo Kikuu cha Michigan

Sasha Obama alianza mafunzo katika Chuo Kikuu cha Michigan mwaka jana.

Ni mtoto wa Obama ambaye amekwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha kawaida katika familia ya Obama , kwani dada yake kwa sasa anasomea katika Chuo Kikuu cha Harvard, mama yake alisomea katika Princeton na Barack Obama alisomea Chuo Kikuu cha Columbia Ukabla ya kusomea katika chuo cha sheria cha Harvard

Yeye na Malia wanaendelea na masomo nyumbani kwa njia ya mtandao kutokana na janga la Corona.

Di Oba,mas

Sasha anaonesha picha ya mama yake katika makala ya Michelle Obama

Mke wa rais wa zamani wa Marekani , Michelle Obama alitoa toleo la makala kuhusu maisha yake inayoitwa , “Becoming” mwezi mei , ambayo alimshirikisha Sasha.

Waandishi wa habari wanasema makala hiyo ilionesha kwa kina zaidi maisha ya watoto hao wawili wa rais wa zamani wa Marekani ambapo Sasha anaelezea kuwa watu wanapaswa kujivunia jinsi walivyo.

Ndiye mwenye chumba kikubwa zaidi ndani ya nyumba ya baba yake

katika mahojiano ya hivi karibuni Bi Michelle Obama alisema kuwa watoto wake wawili wanaendelea na masomo kwa njia ya mtandao kutokana na janga la virusi vya corona na akasema Sasha ndiye mwenye chumba kikubwa zaidi cha kulala katika nyumba yao.

Alipoulizwa Je chumba hicho kina ukubwa gani ? Bi Michelle Obama alisema chumaba cha Sasha kina ukubwa sawa na sebule yao ambacho hukitumia kama darasa kwasababu sasa corona imewalazimisha kusomea nyumbani.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *