img

Msanii wa filamu Mzee Jengua afariki dunia

December 15, 2020

 

Chama cha waigizaji Dar Es Salaam Tanzania, kimetangaza kifo cha msanii maarufu wa filamu Mzee Jengua ambaye amefariki dunia siku ya leo Disemba 15 majira ya asubuhi nyumbani kwa mtoto wake Mkuranga.

Aidha taarifa hizo zimethibitishwa na mke wake na taarifa kuhusu mipango ya mazishi wanasubiria vikao vya familia ili kutoa ratiba kamili ya mazishi hayo.

EATV & EA Radio Digital, imepiga stori na msanii wa filamu Steve Nyerere na amemzingumzia Mzee Jengua ambaye waliwahi kufanya filamu moja ya Mke mwema.

“Taarifa tumezipokea tunasubiria vikao vya familia yake ili tukampumzishe mzee wetu, unapotamka Jengua unakuwa umetaja jina kubwa sana kwenye soko la filamu hapa nchini Tanzania, alikuwa mcheshi sana,ukimuangalia hachoshi na ana vituko vingi, mimi nimecheza naye filamu moja ya Mke mwema na alikuwa kama baba mkwe wangu” ameeleza Steve Nyerere

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *