img

Marekani yaiwekea vikwazo Uturuki kutokana na silaha za Urusi

December 15, 2020

Dakika 5 zilizopita

Moonyesho ya mfumo wa ulinzi wa makombora ya masafa - S-400 missile
Maelezo ya picha,

Moonyesho ya mfumo wa ulinzi wa makombora ya masafa – S-400 missile

Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya mshirika wake wa Nato Uturuki kutokana na kitendo chake cha hatua yake ya kununua mfumo wa ulinzi makombora ya masafa marefu uliotengenezwa na Urusi ambao iliununua mwaka jana.

Marekani inasema kuwa matumizi ya mfumo huo- S-400 ni kinyume na teknolojia ya Nato na ni tisho kwa washirika wake wa maeneo ya Ulaya na Atlantiki.

Vikwazo hivyo vilitangazwa na wizara ya mambo ya nje Jumatatu vinalenga sekta ya Uturuki ya ununuzi wa silaha.

Hatua hiyo ya vikwazo imelaaniwa vikali na maafisa wa Uturuki na Urusi and Russia.

Marekani ilikuwa tayari imekwisha iondoa Uturuki katika mpango wake wa ndege za kivita F-35 za aina ya jet kwasababu Uturuki ilinunua mfumo wa makombora ya masafa marefu kutoka Urusi

Ni lipi lengo la Marekani ?

Waziri wa ulinzi wa Marekani Mike Pompeo ameitaka uturuki iachane na makombora ya Urusi
Maelezo ya picha,

Waziri wa ulinzi wa Marekani Mike Pompeo ameitaka uturuki iachane na makombora ya Urusi

“Marekani imekuwa muwazi kwa Uturuki kwa viwango vya juu na mara nyingi kwamba ununuzi wake wa mfumo wa makombora wa S-400 utahatarisha teknolojia ya kijeshi ya Marekani na wanajeshi wake na unaipatia fedha nyingi sekta ya ulinzi ya Urusi, pamoja na kuiwezesha Urusi kuingilia utendaji wa vikosi vya Uturuki na sekta ya ulinzi kwa ujumla ,” taarifa ya Waziri wa ulinzi wa Marekani Mike Pompeo ilisema.

“Uturuki hatahivyo iliamua kutoisikiliza tahadhari ya Marekani na ikaendelea na mpango wake wa kununua na kufanya majaribio ya S-400, licha ya uwepo wa mifumo mingine mbadala inayokubalika miongoni mwa washirika wa Nato inayofahamika kama- Nato-interoperable systems ,” aliendelea kusema Bw Pompeo.

“Ninaitaka Uturuki kusuluhisha tatizo la S-400 mara moja kwa ushirikiano na Marekani ,” alisema. “Uturuki ni mshirika wa maana na mshirika muhimu wa Marekani katika masuala ya usalama wa kikanda, na tunataka akuendelea na historia yetu ya miongo ambayo imetuwezesha kuwa na ushirikiano wa manufaa kwa kuondoa kikwazo cha umiliki wa Uturuki wa mfumo wa S-400 haraka iwezekanavyo.”

Vikwazo vinawalenga rais wa idara ya viwanda vya ulinzi wa Uturuki Ismail Demir, na wafanyakazi wengine watatu.

Vikwazo hivyo ni pamoja na marufuku ya vibali vya uagizwaji wa bidhaa kutoka Marekani, pamoja na kufujwa kwa mali zao zilizopo nchini Marekani.

Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imeitaka Marekani “kuangalia upya uamuzi wake usio wa haki kama ilivyotakazwa leo “, na kuongeza kuwa Uturuki “iko tayari kutatua tatizo hili kwa njia ya mazungumzo na diploamasia kwa kulingana na matakwa ya muungano wa Nato”.

Wizara hiyo ilionya kuwa vikwazo vya Marekani “bila shaka vitakuwa na athari mbaya kwa mahusiano yetu , na Uturuki itajibu ka jia na muda itakaoona unafaa “.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov pia amelaani uamuzi wa Marekani dhidi ya Uturuki

Maelezo ya picha,

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov pia amelaani uamuzi wa Marekani dhidi ya Uturuki

Uongozi wa Ankara unadai kuwa mfumo huo wa Urusi ulinunuliwa baada ya Marekani kukataa kuiuzia makombora yake ya masafa marefu. Maafisa wa walisema kuwa Ugiriki – ambayo ni mshirika mwingine wa Nato – ina mfumo wake binafsi wa S-300, inagawa haukununuliwa moja kwa moja kutoka Urusi.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov pia amelaani uamuzi wa Marekani dhidi ya Uturuki akiutaja kama “dhihirisho jingine la tabia ya Marekani ya kiburi kuhusu sheria ya kimataifa.

“Dhihirisho la uchukuaji wa hatua zisizo za kisheria, hatua za kimabavu ambazo Marekani imekuwa ikizitumia kwa miaka mingi , tayari miongo, kushoto na kulia ,” Aliendelea kusema Bw Lavrov

line

Je Uturuki ina umuhimu gani?

Uturuki ina kikosi kikubwa katika Nato, wajumbe 30 wa muungano.

Ni mmoja wa washirika muhimu wa Marekani , na ipo katika eno muhimu kimkakati, ikipakana na mataifa ya Syria, Iraq na Iran.

Pia imekuwa na jukumu muhimu katika mzozo wa Syria, kwa kutoa wanajeshi nausaidizi wa kijeshi kwa baadhi ya makundi ya waasi wanaoungwa mkono na Nato.

Hatahivyo, uhusiano wake na baadi ya mataifa wanachama wa Nato na Muungano wa Ulaya umekuwa ukidorora , ambao wamekuwa wakimshutumu Bw Erdogan kuongoza kiimla kufuatia kushindwa kwa jaribio la mapinduzi dhidi yake mwaka 2016.

line

Mfumo wa makombora wa S-400 unatumikaje?

Diagram of how S-400 missile system works
  • Ni mfumo wa masafa marefu wa upelelezi unaoshambulia vifaa na kurusha taarifa katika gari maalum ambalo hutathmini maeno yanayoweza kulengwa na makombora hayo.
  • Eneo linalolengwa hutambuliwa na gari maalum huamuru kombora kurushwa
  • Taarifa za kurushwa kwa kombora hutumwa katika eno bora na kuachilia kombora la anga
  • Rada ya mawasiliano husaidia kuongoza makombora kwenye eneo linalolengwa

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *