img

Magaidi 20 wa kundi la Boko Haram wauawa na jeshi la Nigeria

December 15, 2020

Wanamgambo 20 wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameripotiwa kuangamziwa kwenye operesheni iliyofanyika nchini Nigeria.

Kundi hilo la kigaidi la Boko Haram lilikuwa likijaribu kuendesha shambulizi kwenye mkoa wa Askira Uba jimbo la Borno.

Naibu Msemaji wa Kikosi cha Jeshi la Nigeria Ado Isa, alitangaza kuwa shambulizi hilo lilizuiliwa  kutekelezwa, na magaidi 20 waliuawa huku magari 4 ya silaha yaliyomilikiwa na kundi hilo yakikamatwa.

Mwanajeshi 1 alipoteza maisha na wengine 2 wakajeruhiwa katika operesheni hiyo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *