img

Madiwani waapishwa wajadili utekelezaji wa shuguli za halmashauri

December 15, 2020

Na Timothy Itembe MARA.

MADIWANI wa halmashauri ya mji wa Tarime mkoan Mara wamejadili taarifa ya ya mkurugenzi ya utekelezaji wa shuguli kipindi ambacho waheshimiwa madiwani hawakuwepo Julai-Novemba 2020.

Moja ya maeneo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na maelezo mafupi,haliyakijografia ya halmashauri,eneo la utawala na idadi ya watu,hali yahewa,hali ya kisiasa,hali ya utekelezaji wa shuguli mbalimbali za halmashauri,idara ya utawala na utumishi,idara ya fedha,idara ya mipango Takwimu na ufuatiliaji,idara ya kilimo na ushirika,jumla zikiwa Arobaini.

Akiongoza kikao hicho mwenyekiti mpya Daniel Komote ambaye alichaguliwa aliwataka madiwani kupokea na  kujadili taarifa hiyo na pale ambao kutakuwa kuna changamoto itahitajika kurudi ndani ya kamati husika ili kujadiliwa na kupata majibu ya kina ikiwemo kupata utatuzi wake.

Mbali na mwenyekiti wengine aliohoji katika taarifa hiyo nipamoja na Mbunge viti maalumu,Ghati Chomete ambaye aliwataka madiwani pamoja na watumishi kushirikiana ili kuiletea halmashauri hiyo maendeleo.

“Niwaombe ndugu zangu tuungane pamoja ili kuiletea halmashauri maendeleo pamoja na hayo niwaombe madiwani wenzangu kwenda kukaa na wananchi waliowachagua ili kuibua miradi katika maeneo yenu kuja kujadiliwa katika utekelezaji wake jambo ambalo olitafanikisha kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wetu”alisema Chomete.

Naye diwani kata ya Turwa Chacha Marwa Machugu maarufu Chacha Musukuma aliwatetea wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Machinga kuwa wasiondolewe  mbele ya vibanda vya wafanyabiashara wanakotandika bidhaa zao na badala yake waandaliwe mazingira na maeneo mengine ya kufanyia biashara ndipo waondolewe katika maeneo hayo ya Soko jipya la Rebu.

 Katika hafla hiyo madiwani 11 akiwemo Mbunge wa jimbo la Tarime mjini,Michael Kembaki pamoja na Mbinge viti maalumu Mara,Ghati Chomete walipokea kiapo cha utii ambapo Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya Tarime,Vincencia Balyaruha aliwataka kuzingatia kiapo walichokula na  wasikengeuke.

Wakati huo huo Godson Kweka katibu msaidizi Sekeretariet ya maadili ya viongozi kanda ya Ziwa aliwapitisha kula kiapo cha utii wa utumishi wa umma na kuwaahidi kuwaletea mafunzo ya utumishi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *