img

Kocha wa zamani Houllier afariki dunia akiwa na umri wa miaka 73

December 15, 2020

 

Vilabu viwili vya Ufaransa – PSG na Lens ambavyo Houllier aliviongoza vimethibitisha kifo hicho. Alikuwa Liverpool kuanzia 1998 to 2004, alifariki usiku wa kuamkia leo wakati akifanyiwa upasuaji wa moyo. Amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya.

Katika Premier League ya England, macho yataelekezwa katika mtanange wa Jumatano wakati mabingwa Liverpool watawakaribisha vinara Tottenham Hotspur dimbani Anfield huku timu hizo zikitenganishwa tu na tofauti ya mabao.

Timu hizo ziliteleza mwishoni mwa wiki baada ya Spurs kutoka sare ya 1 – 1 na Crystal Palace nao Liverpool wakahitaji penalty ya dakika za mwisho ili kupata pointi moja katika sare ya 1 – 1 dhidi ya washika mkia Fulham. Nje ya uwanja, mpambano wa makocha kati ya Special One Jose Mourinho na Normal One Jurgen Klopp unaongeza utamu kwa mtanange huo ambao utatizamwa na mashabiki 2,000 ndani ya Anfield.

AFP/reuters/DPA/AP

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *