img

Waziri mkuu wa Eswatini afariki dunia

December 14, 2020

Waziri mkuu wa Eswatini, utawala wa mwisho kabisa wa kifalme wa Afrika, alifariki dunia katika hospitali moja ya Afrika Kusini Jumapili baada ya kuambukizwa virusi vya na corona, serikali ilisema katika taarifa.

Ambrose Dlamini, 52, alikuwa amelazwa katika nchi jirani ya Afrika Kusini mwanzoni mwa Desemba, wiki mbili baada ya kupimwa na kukutwa na ugonjwa wa Covid-19.

“Wakuu wameamuru kwamba nijulishe taifa juu ya kifo cha kusikitisha na cha mapema cha Mheshimiwa Waziri Mkuu Ambrose Mandvulo Dlamini,” Naibu Waziri Mkuu Themba Masuku alisema.

Waziri mkuu “alifariki mchana huu akiwa chini ya uangalizi wa matibabu katika hospitali moja nchini Afrika Kusini,” akaongeza, bila kuelezea sababu ya kifo cha Dlamini.

Dlamini alikuwa ametangaza katikati ya Novemba kwamba alikuwa amekutwa na virusi vya corona lakini akasema kwamba alijisikia vizuri na alikuwa hana dalili.

Imetayarishwa na Sunday Shomari VOA, Washington DC

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *