img

Watu 14 wamefariki ajalini

December 14, 2020

Watu 14 wamepoteza maisha na wengine 13 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea maeneo ya Kiini cha Mkiwa mkoani Singida iliyohusisha gari ndogo ya abiria na Lori lililokua linatokea Dar es Salaam kwenda Kahama.

Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Sweetbert Njewika, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akidai kuwa chanzo ni uzembe wadereva wa gari ya abiria ambae alikua Mwendokasi.

“Dereva wa gari ndogo ya abiria alikuwa Mwendokasi sana, akaovertake Lori bila taadhari.” Njewika

Amesema katika ajali hiyo dereva wa gari la abiria ni miongoni mwa waliopoteza maisha na majeruhi wanapatiwa matibabu kwenye hospitali ya Manyoni.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *