img

Wajumbe Marekani wakutana kumchagua rasmi Joe Biden kama rais

December 14, 2020

 

Wajumbe wa jopo maalumu wanaomchagua rais wanakutana leo kote Marekani kumchagua rasmi Joe Biden kama rais wa nchi hiyo. 

Jumatatu kawaida ndiyo siku iliyotengwa kisheria ya kukutana kwa wajumbe wanaopiga kura hiyo. Wajumbe hao wanakutana katika majimbo yote hamsini pamoja na wilaya ya Columbia kupiga kura zao. 

Matokeo ya kura hiyo yatapelekwa Washington ambako yatajumlishwa katika kikao cha pamoja cha bunge la Congress mnamo Januari 6 kitakachoongozwa na makamu wa rais Mike Pence. 

Rais Mteule Joe Biden anatarajiwa kulihutubia taifa usiku wa leo baada ya kura hiyo ya wajumbe. 

Kura hiyo inasubiriwa na wengi kuonekana jinsi itakavyokwenda kwa kuwa Rais Donald Trump amekataa kukiri kushindwa na ameendelea na madai yake yasiyokuwa na ushahidi ya wizi wa kura uliofanyika katika uchaguzi wa Marekani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *