img

Virusi vya corona: Maafisa wa White House kupokea chanjo ya Pfizer

December 14, 2020

Dakika 9 zilizopita

President Donald Trump speaks during a news conference with Vice President Mike Pence

Maelezo ya picha,

Rais Donald Trump amesema awamu ya kwanza ya chanjo hiyo itapewa wafanyakazi wa White House waliyo na mahitaji maalum ya kiafya

Maofisa wa ngazi ya juu katika utawala wa Trump watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza watakaopewa chanjo ya corona, maafisa nchini Marekani wamesema.

Maafisa wamesema baadhi ya wafanyakazi wa White House wanatarajiwa kupewa chanjo ya Pfizer/BioNTech wiki hii.

Lakini siku ya Jumapili, Rais Donald Trump alisema chanjo ya mapema itatolewa kwa watu maaluma.

Chanjo hiyo inatoa ulinzi wa hadi asilimia 95 dhidi ya Covid-19 ana inaidhinishwa kuwa salama na wadhibiti wa dawa wa Marekani iliyopita Ijumaa.

Dozi milioni tatu za kwanza za chanjo hiyo kwasaba zinasambazwa katika maeneo tofauti katika majimbo yote 50 ya Marekani.

Shehena ya kwanza ya dozi hizo iliwasilishwa Michigan siku ya Jumapili, wahudumu wa afya na wazee ndia wanaotarajiwa kupewa mapema Jumatatu.

Vifo vilivyotokana na corona vimeongezeka sana mwezi Novemba nchini Marekani, ikivunja rekodi duniani kwa kuwa na idadi ya juu zaidi ya maambukizi ya 3,309 siku ya Jumamosi.

Lakini kuzinduliwa kwa mpango wa chanjo kunachukuliwa kuwa hatua kubwa katika mapambano dhidi ya janga la corona, ambalo limesababisha vifo vya watu 300,000 Marekani.

Chanjo

Mamlaka ya chakula na dawa (FDA) imesema kuwa imeamua kuidhinishwa chanjo ya dharura, katika tangazo lake la Ijumaa kama “hatua muhimu” katika jitihada za kukabiliana janga la corona, baada ya utawala wa Marekani kushinikizwa vikali kuidhinisha chanjo hiyo.

Mpango wa kutoa chango kama hiyo unaendelea nchini Uingereza. Chanjo ya Pfizer pia imeidhinishwa nchini Canada, Bahrain na Saudi Arabia.

Ni maafisa wapi watakaopewa chanjo White House?

Baadhi ya chanjo za kwanza zimetengewa watu waliofanya kazi kwa karibu na Bwana.Trump, mafisa wameambia vyombo kadhaa vya habari nchini Marekani.

Lakini baadae chanjo hiyo itapewa maofisa wa vitengo vitatu vya serikali, ikiwa ni pamoja na White House, Congress na Mahakama ya Juu Zaidi.

Afisa mmoja ambaye jinalake halikutajwa ameambia Shirika la Habari la Reuters kwamba chanjo itahakikisha serikali inaweza “kuendelea na kutekeleza shughuli zake muhimu, bila kukatizwa “.

White House Chief of Staff Mark Meadows (C) as he walks to a meeting with Republican Senate Majority Leader Mitch McConnell

Maelezo ya picha,

Mkuu wa wahudumu wa White House Mark Meadows ni miongoni mwa watu wa karibu na Rais Trump ambao waliambukizwa Covid-19

Mpango huo wa chanjo ambao kwanza uliripotiwa mara ya kwanza na Gazeti la New yORK Times, umethibitishwa na msemaji wa Baraza la Kitaifa ya Usalama (NSC) John Ullyot siku ya Jumapili.

Lengo kuu la mpango huo ni kujenga imani ya umma kuhusu chanjo hiyo, alisema.

“Watu wa Marekani waamini kuwa wanapokea chanjo salama na inayofanya kazi ambayo piwa imepewa maofisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Marekani kutokana na ushauri wa waataalamu wa afya ya umma na uongozi wa usalama wa kitaifa,” Bw. Ullyot alisema.

Boxes containing Pfizer's vaccine are unloaded from air shipping containers at UPS Worldport, in Louisville, Kentucky

Maelezo ya picha,

Chanjo ya Pfizer zikisafirishwa maeneo tofauti nchini Marekani

Baadaye Jumapili Rais Trump alifafanua katika Twitter yake kwamba “watu wanaofanya kazi White House watapokea chanjo hiyo baadaye katika mpango huo pengine iwe lazima”.

Bw Trump, ambaye aliyeambukizwa virusi vya corona mwezi Novemba na kupona baada ya kutibiwa hospitalini, aliongeza : “Mimi sijapangiwa kupewa chanjo hiyo lakini natazamia kupewa wakati kwafaka ukiwadia.”

Kumekuwa na visa kadhaa vya mlipuko wa virusi vya corona katika Ikulu ya White House, huku maofisa kadhaa wa ngazi ya juu wakiripotiwa kupatikana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Haijabainika, ikiwa Naibu wa Rais Mteule Kamala Harris na wanachama wa kundi lake watapewa chanjo hiyo ya mapema.

Chanjo ya Pfizer/BioNTech ni gani?

Pfizer/BioNtech ni kampuni ya kwanza ya dawa kutoa maelezo kuhusu awamu ya mwisho ya kufanyia majaribio chanjo yake.

Ni aina mpya inayoitwa mRNA inayotumia alama za chembechembe za jeni ya urithi kutoka kwa virusi kuufundisha mwili jinsi ya kupamabana na Covid-19 na kujenga kinga ya mwili.

Chanjo ya mRNA haijawahi kuidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu awali, japo watu wamekuwa wakiipokea katika majaribio ya kimatibabu katika kliniki. Chanjo hii ni lazima itunzwe katika mazingira ya takriban nyuzi joto chini ya 70 na itakuwa ikisafirishwa katika maboksi maalum, yaliyowekwa katika barafu kavu.

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Changamoto anazokabiliana nazo mhudumu wa afya dhidi ya corona

Pale inapofikishwa katika eneo husika, inaweza kutunzwa hadi kwa muda wa siku tano ndani ya friji.

Matokeo yake inaashiria kuwa chanjo hiyo inaweza kumkinga mtu kutokana na Covid- 19 kwanza asilimia 90.

Karibu watu 43,000 wamepewa chanjo hiyo na hakuna visa vya hofu ya usalama wake vilivyoripotiwa.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *