img

Urusi yakanusha kuhusika na udukuzi katika wizara za fedha na biashara Marekani

December 14, 2020

 

Ikulu ya Kremlin imesema leo kuwa Urusi haikuhusika kabisa na udukuzi uliofanyika katika wizara za fedha na biashara nchini Marekani. 

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amepuuzilia mbali madai yote yaliyoihusisha Urusi na tukio hilo akisema Rais Putin ndiye aliyeipendekezea Marekani kukubali na kumaliza makubaliano ya usalama wa kimtandao na Urusi. 

Watu walio na taarifa za ndani kuhusiana na udukuzi huo wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa wadukuzi wanaaminika kuifanyia kazi serikali ya Urusi na kuna hofu kwamba udukuzi huo uliofanyika sasa ndio mwanzo tu wa mkoko kualika maua. 

Mtu mmoja anayehusika na suala hilo anasema udukuzi huo ulikuwa mkubwa kiasi cha kwamba ulisababisha kufanyika kwa mkutano wa Baraza la Kitaifa la Usalama katika ikulu ya Marekani White House Jumamosi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *