img

Uingereza na Umoja wa Ulaya kuendelea na mazungumzo ya Brexit licha ya muda wa mwisho kupita

December 14, 2020

 

Umoja wa Ulaya na Uingereza zitarudi kwenye meza ya mazungumzo leo baada ya kukubaliana kutozingatia muda wa mwisho wa mazungumzo ya kupata mwafaka kuhusiana na Brexit. 

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Urusula von der Leyen pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson juma lililopita walisema wataamua iwapo kuna uwezekano wa kupata maelewano ifikiapo jana Jumapili ila wakakubaliana pia kwenda hatua zaidi. 

“Timu zetu zinazohusika na majadiliano zimekuwa katika mazungumzo usiku na mchana katika siku za hivi karibuni na licha ya uchovu ulioko baada ya karibu mwaka mmoja wa majadiliano na licha ya kuwa hakujapatikana maelewano katika muda uliokuwa umewekwa, kwa sasa sote tunafikiri ni jambo la busara kwenda hatua zaidi. 

Tumeziagiza timu zetu kuendelea na mazungumzo ili kuona iwapo makubaliano yatapatikana hata katika hatua kama hii.

“Kiongozi wa majadiliano hayo upande wa Umoja wa Ulaya Michel Barnier na mwenzake wa Uingereza David Frost walifanya mazungumzo Jumamosi na jana Jumapili. 

Wamekuwa wakisafiri London na Brussels ila kwa sasa inaripotiwa kuwa mazungumzo hayo yatafanyika tu mjini Brussels.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *