img

Uhuru wa vyombo vya habari uko wapi?

December 14, 2020

Kupitia ripoti ya kila mwaka iliyochapishwa leo Jumatatu, Katja Gloger mwenyekiti wa Waandishi wa Habari wasio na Mipaka Ujerumani (ROG), amesema kuwa kusema kweli, ni sehemu ya kwanza inayohusika na kufungwa, kutekwa nyara na kupotea kwa waandishi wa habari. Kufikia Disemba 1 wafanyikazi wa vyombo vya habari 387 wapo gerezani.Waandishi 49 wameuwawa kwa mwaka 2019

Ripoti hiyo aidha inadokeza kuwa sehemu ya pili itachapishwa muda mfupi kabla ya Mwaka Mpya ikiangazia idadi ya waandishi wa habari ambao wameuwawa huku  “Nyuma ya kila moja ya kesi hizo ikiwa ni hatima ya mtu anayetishiwa na kesi za jinai, kifungo cha muda mrefu na unyanyasaji mara nyingi kwa sababu hawakukubali udhibiti na ukandamizaji.

Mwandishi wa habari Sylvie Ahrens-Urbane anatolea mifano halisi kutoka Afrika. Mwandishi habari maarufu wa uchunguzi Hopewell Chin’ono kutoka Zimbabwe alikuwa amechunguza uuzaji wa dawa za COVID-19 kwa bei za juu na serikali. Alikamatwa kikatili kutoka nyumbani kwake, amesalia gerezani kwa muda wa mwezi mmoja na nusu sasa huku ombi la kuachiliwa kwa dhamana likikataliwa mara kadhaa.

Reporter Ohne Grenzen Iran Aktivist Protest

Mwanaharakati wa Waandishi wa Habari wasio na Mipaka

Kesi ni nyingi

Na sio kesi hiyo pekee pia mwandishi habari wa Rwanda Dieudonné Niyonsenga bado yupo chini ya ulinzi. Mkurugenzi wa kituo cha runinga kupitia mtandao cha “Ishema” anatuhumiwa kwa kupuuza kanuni za nchi hiyo za Corona. Corona yatishia uhuru wa habariKulingana na habari kutoka kwa “Waandishi wa Habari wasio na Mipaka”, Niyonsenga alikuwa tayari amekamatwa mnamo Aprili baada ya kuripoti juu ya athari za kanuni za serikali juu ya maisha ya umma. Kulingana na mtaalam wa Afrika Ahrens-Urbane,  serikali ya Rwanda, inasema madai ya Niyonsenga kwamba wanajeshi walifanya ubakaji wakati wa kutekeleza amri ya kutotoka nje yalivuka mipaka.

Taarifa hiyo inasema kuwa waandishi habari wengi waliofungwa wako China. Kulingana na Waandishi Wasio na Mipaka, kesi kutoka Rwanda na Msumbiji zinathibitisha mwelekeo wa ulimwengu,  Ingawa Afrika ilikumbwa na matokeo ya janga la Corona baadaye kuliko Asia na Ulaya na mashambulio juu ya uhuru wa vyombo vya habari pia yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya Corona.

Pressefreiheit Symbolbild

Wanaharakati wakiwa wamefungwa minyororo mikononi wakati wa maandamano nje ya ubalozi wa Misri

Misri ni nchi ya Kiafrika yenye waandishi wengi wa habari gerezani

Ahrens-Urbane amedokeza kuwa wakati virusi vya corona vilisambaa kwa haraka, mara tatu idadi ya waandishi wa habari waliishia gerezani kuanzia Machi 15 hadi 15 Mei kuliko mwaka mmoja uliopita. Mwisho wa Novemba, jumla ya wanaume na wanawake 40 walikuwa wamekamatwa kwa sababu ya kuripoti juu ya janga hilo.

Kuangalia ramani ya ulimwengu, Misri ni nchi ya Kiafrika yenye waandishi wengi wa habari gerezani ambao ni 30, na China ina waandishi habari 117 gerezani. Idadi jumla katika nchi zote kufikia Disemba 1 ilikuwa 387.

Waandishi wa habari wanawake wanazidi kuishia gerezani kutokana na kazi yao na kufikia sasa, 42 wameathiriwa, asilimia 35 zaidi kuliko mwaka 2019.Ripoti ya mwaka 2007 ya Waandishi wasio na mipaka

Takwimu zinaashiria kuwa kufikia sasa kuna waandishi wa habari 54 mikononi mwa watekaji, walioenea katika nchi tatu zilizoghubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambazo ni Syria, Iraq, Yemen. “Waandishi habari Wasio na Mipaka wamejitolea kushinikiza kuachiliwa kwa waandishi wote waliotekwa nyara na waliopotea katika mazingira tofauti.

 

/http://www.dw.com/a-55926770

 

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *