img

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 14.12.2020: Alli, Isco, Zidane, Khedira, Rondon, Depay, Dybala,

December 14, 2020

Dakika 2 zilizopita

Sami Khedira

Maelezo ya picha,

Sami Khedira athibitisha kuzungumza na Everton

Kiungo wa kati wa Juventus Mjerumani Sami Khedira, 33, ambaye anapanga kuhama klabu hiyo mwezi Januari, amethibitisha kuwasiliana na mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti. (Bild – in German)

Everton wako tayari kumpatia ofa ya uhamisho wa bila malipo kiongo wao wa kati Dele Alli, 24 mwezi Januari kwa lengo la kuikosesha Tottenham Hotspur nafasi ya kumsajili. (Star)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema kuwa kiongo wa kati Mhispania Isco hayuko katika mipango yake ya siku zijazo. Hata hivyo, kiungo huyo aliye na umri wa miaka 28-anatarajiwa kuondaka klabu hiyo mwezi Januari. (Marca – in Spanish)

Isco

Mshambuliaji wa Venezuela Salomon Rondon, 31, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Dalian Pro, China amehusishwa na tetesi za kuhamia Wolves kushikilia nafasi ya Raul Jimenez aliyejeruhiwa. (Sun)

Paris St-Germain huenda ikamsajili mshambuliaji wa Lyon Mholanzi Memphis Depay msimu ujao lakini Barcelona wamekuwa wakimnyatia kwa muda mrefu kiongo huyo aliye na umri wa miaka 26. (Le Parisien – in French)

Tottenham wako tayari kulipa Juventus £63.6m kumunua mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27. (TodoFichajes – in Spanish)

Paulo Dybala

Maelezo ya picha,

Tottenham wako tayari kulipa Juventus £63.6m kumnunua Paulo Dybala

Kiungo wa kati wa Lyon Mfaransa Houssem Aouar, 22, ambaye amekuwa akinyatiwa kwa muda mrefu na Arsenal, pia analengwa na Paris St-Germain huku klabu hiyo ikitarajiwa kuanza mazungumzo kumhusu mchezaji huyo hivi karibuni. (RMC – in French)

Klabu za Leeds na West Ham ni miongoni mwa Ligi ya Primia ambazo zinamsaka mlinzi wa MK Dons Matthew Sorinola,(Teamtalk)

Tetesi za Soka Jumapili

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, amedokeza kuwa nafasi ya yeye kuondoka Paris St-Germain itategemea ridhaa ya wazazi wake. (Copa 90, via Sun on Sunday)

Mshambuliaji wa Ufaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta hajamkataa mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil anayechezea kikosi cha washika bunduki kabla ya mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 32 kumalizika msimu huu. (Star on Sunday)

United tayari wamekataa mpango wa kubadilishana na Juve wakiwahusisha winga Douglas Costa, 30, na kiungo wa kati wa Barcelona Miralem Pjanic,30, ili kumnasa Pogba. (Calciomercato)

Juventus wana matumaini kuwa Manchester United watamruhusu kiungo wa kati Paul Pogba, kurejea Turin

Chelsea wanajitahidi kutafuta wanunuzi wa kipa Kepa Arrizabalaga, 26, beki wa kushoto Mhispania Marcos Alonso, 29, na mlinzi wa Kidenmark Andreas Christensen, 24, ambao wote watapatikana mwezi Januari. (Sunday Express)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameghairi chakula cha mchana wakati wa sikukuu ya Krisimasi kwa sababu ya hofu ya Covid-19. (Sunday Mirror)

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *