img

Shambulio la shule Nigeria: Majambazi waliowateka watoto Katsina ‘wazingirwa’

December 14, 2020

Dakika 6 zilizopita

Police members are deployed after gunmen abducted students from the all-boys Government Science school in Kankara, in northwestern Katsina state, Nigeria December 13, 2020

Maelezo ya picha,

Usalama umeimarishwa katika shule hiyo kufuati amashambulio hayo

Wanajeshi wa serikali wamezingira eneo ambalo watu waliojihami kwa bunduki wanaaminiwa kuwashikilia mateka watoto wa shule katika eneo la kaskazini – magharibi mwa Nigeria, msemaji wa Rais Muhammadu Buhari amesema.

Watoto 10 wameripotiwa kushikiliwa mateka, Garba Shehu amesema, idadi ambayo ni ndogo kuliko ile iliyoripotiwa na wafanyakazi kutoweka.

Karibi wanafunzi 800 wanasoma katika shule hiyo ya bweni ya wavulana katika jimbo la Katsina na karibu nusu yao hawajulikani waliko.

Washambuliaji wanasadikiwa kutaka kulipwa kikombozi, Bwana Shehu amesema.

Serikali imetaja washambuliaji hao kuwa majambazi, jina linalotumika kuashiria genge linalohudumu katika eneo hilo.

Shirika la kutetea haki la Amnesty International linasema watu 1,100 waliuawa na majambazi kaskazini mwa Nigeria katika mizi sita ya kwanza ya mwaka huu, lakini serikali imeshindwa kuwachukulia hatua washambuliaji hao.

Parents gather during a meeting at the Government Science school after gunmen abducted students from it, in Kankara, in northwestern Katsina state, Nigeria December 13, 2020

Maelezo ya picha,

Wazazi walifika shuleni kusubiri taarifa kuhusu hali ya watoto wao

Mwandishi wa BBC Nigeria Mayeni Jones amesema kumekua na ongezeko la wasiwasi kuhusu hali ya usalama nchini Nigeria.

Eneo la kaskazini – magharibi limeathiriwa zaidi na utekaji wa kutafuta kikombozi, eneo la kaskazini mashariki linahangaishwa na wanamgambo wa Kislamu, huku eneo la kusini likikabiliwa na mashambulio kutoka kwa makundi yanayolenga viwanda vya mafuta vikitaka mgao wa mapato ya mafuta, aliongeza kusema.

Wazazi wamekusanyika katika shule hiyo iliyopo eneo la Kankara, wakitoa wito kwa mamlaka kuwasaidia kuwapata watoto wao, Shirika la habari la Reuters limeripoti.

Mzazi Abubakar Lawal alinukuliwa kusema kwamba watoto wake watatu waliokuwa wakisoma katika shule hiyo hawajulikani waliko.

Majambazi watakabiliwa vikali

Siku ya Jumamosi, jeshi la nchi hiyo lilisema limegundua maficho ya majambazi hao katika msitu mmoja na kukabiliana nao.

Katika mahojiano ya BBC, Bwana Shehu alisema wanajeshi kadhaa “wamepelekwa” katika eneo hilo kuwakomboa watoto hao.

“Makamanda wa kijeshi wanaoongoza oparesheni hiyo wana taarifa kuhusu ni wapi majambazi hao wanaaminiwa kuwa na wanawazuilia watu wangapi. Wamezingira eneo hilo lote ,” aliongeza.

Rais Buhari anatoke jimbo hilo, na kwasasa yuko huko katika ziara ya kibinafsi

Amekuwa akipokea taarifa ya kila baada ya saa kuhusu tukio hilo na juhudi za kuwaokowa wanafunzi waliyotekwa, Bwana Shehu amesema.

“Magenge ya wahalifu na majambazi yatakabiliwa vikali. Yatatokomwezwa,” aliongeza.

Wanafunzi wanaamini wanaamini wenzao 10 walichukuliwa na majambazi hao, lakini bado tunajitahidi kuthibitisha hilo, Bwana Shehu aliongeza kusema.

Mamlaka ya shule hiyo inazungumza na wazazi kubaini ni wanafunzi wangapi waliorudi nyumbani na ni wangapi wengine ambao bado wametawanyika katika eneo hilo baaada ya kutoroka shambulio hilo.

School sign

Maelezo ya picha,

Shule hiyo iko eneo la vijijini katika eneo la kaskazini -magharibi mwa Nigeria

Wakazi wanaoishi karibu na shule hiyo wameambia BBC kwamba walisikia milio ya risasi katibu saa tano usiku (22:00 GMT) wa Ijumaa na kwamba mashambulio hayo yalidumu kwa zaidi ya saa moja.

Walinda usalama katika shule hiyo walijaribu kukabiliana na baadhi ya washambuliaji hao kabla ya polisi kufika, amaafisa walisema.

Polisi wanasema wakati wa makabiliano hayo baadhi ya watu hao waliokuwa wamejihami kwa bunduki walilazimika kurudi nyuma. Wanafunzi walifanikiwa kuruka uwa wa shule na kukimbilia maeneo salama, walisema.

line

Wakazi kadhaa katika eneo hilo wameungana na polisi katika juhudi za kuwatafuta wanafunzi hao, huku baadhi ya wazazi wakiripotiwa kuwaondoa watoto wao katika shule hiyo.

“Shule imesalia mahame, wanafunzi wote wameondoka,” mmoja wa mashuhuda, Nura Abdullahi, aliambia Shirika la habari la AFP.

Gavana wa Katsina, Aminu Bello Massari, ameamuru kufungwa mara moja kwa shule zote za mabweni katika jimbo hilo.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *