img

Serikali ya Ethiopia yatangaza kurejesha mawasiliano tena Tigray

December 14, 2020

 

Ethiopia leo imesema kuwa nguvu za umeme na mawasiliano ya simu yamerudi tena huko Tigray ingawa katika baadhi ya sehemu tu baada ya wiki sita za huduma hizo kuzimwa. 

Serikali hiyo imesema huduma za simu zimerejeshwa katika miji mingine yote isipokuwa Mekele ila nguvu za umeme bado ni changamoto nje ya mji huo mkuu wa Tigray. 

Raia wa Tigray, mji wenye idadi ya watu nusu milioni, wamefurahia kuwasiliana na wapendwa wao kwa mara ya kwanza baada ya wiki kadhaa huku wengine wakijaribu kuwatafuta wale wasiojulikana waliko. 

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alitangaza ushindi dhidi ya wanajeshi wa chama cha TPLF mnamo Novemba 28 baada ya kuuteka mji wa Mekele ambapo anasema aliupata ushindi huo bila mauaji au majeruhi ya raia.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *