img

Rais wa Iran asema Israel ndiyo iliyomuua mwanasayansi wake wa nyuklia

December 14, 2020

 

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema kuwa Israel ndiyo iliyohusika na mauaji ya mwanasayansi aliyeanzisha mpango wa nyuklia wa jamhuri hiyo ya kiislamu katika miaka ya 2000. Rouhani anasema Israel ilimuua ili ianzishe vita katika siku za mwisho za utawala wa Rais Donald Trump. 

Matamshi haya ya rais huyo wa Iran ndiyo ya kwanza yanayoLituhumu taifa hilo la Kiyahudi moja kwa moja na mauaji ya Mohsen Fakhrizadeh mwishoni mwa mwezi uliopita. Israel ambayo kwa muda imeshukiwa kuhusika na mauaji hayo imekanusha kulizungumzia suala hilo. 

Rouhani ameapa kulipiza kisasi ila amesema hatokubali Israel iichagulie wakati na pale itakapofanya shambulizi hilo. Amesema Iran haitokubali kuyumba kwa usalama katika kanda ya Mashariki ya Kati.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *