img

Kocha wa zamani wa klabu ya Liverpool afariki dunia

December 14, 2020

 

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Liverpool Gerard Houllier, amefariki akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na matatizo ya kiafya.

Mfaransa huyo, ambaye pia aliwahi kuifundisha Paris Saint-Germain na Olympique Lyon zote za Ufaransa, alikuwa na historia ndefu ya masuala ya matibabu, haswa shida ya moyo, lakini sababu ya kifo chake bado haijawekwa wazi.

Houllier aliifundisha Liverpool miaka sita kati ya mwaka 1998-2004, alishinda mataji sita ikiwemo mataji manne makubwa, Kombe la Ligi, Kombe la FA na Kombe la Europa League mwaka 2001. na ndio klabu aliyopata nayo mafanikio makubwa katika maisha yake ya ukocha.

Alitumia miaka 38 kama kocha, pia alifundisha timu ya taifa ya Ufaransa mwaka 1992-93, Lyon na Paris Saint-Germain, ambapo alishinda ubingwa wa ligi kuu Ufaransa Ligue 1 mwaka 1986 ambalo lilikuwa taji la kwanza la PSG la ligi kuu kati ya mataji tisa walioshinda mpaka sasa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *