img

Katibu Mkuu UN atoa wito kwa nchi zote kutangaza “dharura ya hali ya hewa”

December 14, 2020

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres alitoa wito kwa nchi zote kutangaza “dharura ya hali ya hewa”.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mzozo wa hali ya hewa uliofanyika kuadhimisha miaka tano ya makubaliano ya hali ya hewa ya Paris, Guterres alisema viongozi wa ulimwengu wanapaswa kutangaza ‘dharura ya hali ya hewa’ katika nchi zao kuchukua hatua ili kuzuia ongezeko la joto duniani.

Guterres alionya kuwa ahadi za sasa za nchi juu ya suala hili “ni mbali na za kutosha” kuweka wastani wa joto kupanda nyuzi 1.5.

Katika hotuba ya Guterres,

“Ikiwa hatutabadilisha mwelekeo wetu, tunaweza kuwa tunaelekea katika janga la joto zaidi ya digrii 3 katika karne hii. Kwa hivyo leo, nawasihi viongozi wote ulimwenguni watangaze Dharura ya Hali ya Hewa.”

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *