img

Halmashauri ya wilaya ya Babatiyamtangaza Mwenyekiti mpya

December 14, 2020

Na John Walter-Babati, Manyara

Baraza la Madiwani la halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara limewapigia kura za kishindo diwani wa kata ya Madunga (CCM) John Noya  kuwa mwenyekiti  wa Halmashauri hiyo huku makamo wake akiwa diwani wa kata ya Ayasanda ,Yahaya Hamisi. 

Mwenyekiti huyo awamu iliyopita alihudumu katika baraza la madiwani kama makamo mwenyekiti akimsaidia majukumu mwenyekiti  wakati huo Nicodemus Tarmo ambaye ameachwa nje msimu huu baada ya kupata  kura chache za maoni ndani ya Chama.

 Uchaguzi huo ulifanyika Dareda makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Babati  mara baada ya madiwani wengine kula kiapo kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa majukumu yao.

 Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo,mwenyekiti wa uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Babati  Halfan Matipula alisema viongozi hao wamechaguliwa na wajumbe kwa asilimia mia moja na hakuna kura zilizoharibika.

 Matipula  aliwataka madiwani hao wahakikishe wanakuwa na mpango mkakati wa kuweka wilaya ya Babati  katika kasi ya maendeleo kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kutekeleza kikamilifu ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020.

 Mkuu wa mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti aliwasisitiza  madiwani hao wawe nyenzo kwa
kutekeleza makujumu yao kwa kuangalia maslahi ya wananchi wao waliowachagua ili kutatua kero zao na sio kutazama maslahi yao binafsi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *