img

Waumini wafanya ibada ya kuiombea Tanzania

December 13, 2020

 Kanisa la Waadiventista wasabato Donge lililopo mtaa wa Makorora Mkoani Tanga limefanya ibada maalumu ya kumshukuru Mungu kwa namna alivyolilinda Taifa na uchaguzi kumalizika kwa amani huku wananchi wakiendelea na shughuli zao za kiuchumi.

Akizungumza mara baada ya ibada ya Sabato ya ujirani mwema mmoja wa wazee wa Kanisa ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa Makorora  Elias Mashika amesema ibada hiyo ni muendelezo wa maombi waliyoyafanya, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu kufanyika.

Amesema walianza kuliombea Taifa kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi kufanyika kwa amani kama maombi walivyofanya wameona ni vyema tena waweze kumshukuru Mungu kwa namna alivyolifanya Taifa kumalizika uchaguzi kwa amani.

Aidha amewashauri viongozi wote wa dini mbalimbali kuendelea kuwaombea viongozi wote waliochaguliwa Mungu aweze kuwatia nguvu waweze kuongoza Taifa kwa amani ili nchi iweze kusonga mbele na hatimaye kuleta maendeleo.

Kwa upande wake mchungaji Hadson Mngumi amesema miezi kadhaa iliyopita, walikuwa na ibada kama hiyo ya, kuombea uchaguzi na kuiombea serikali na kwa namna ya pekee kwa kuwa Mungu amejibu maombi uchaguzi umepita, kwa amani wamechukua fursa hiyo kuliomba Taifa na viongozi walioshika, madaraka katika nyazfa mbalimbali.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *