img

Watu 6 wameuwawa na wengine 24 wametekwa nchini DRC

December 13, 2020

 

Watu sita wameuwawa na wengine 24 wametekwa nyara katika shambulizi lililofanywa na kundi la wanamgambo la ADF kwenye jimbo tete la Kivu Kaskazini, mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Afisa wa serikali kwenye eneo hilo amesema uhalifu huo umetokea kwenye wilaya ya Beni na miongoni mwa watu 24 waliotekwa yumo pia mwandishi habari wa redio moja ya kijamii.

Kundi la wanamgambo la ADF linalaumiwa kwa kuwauwa watu wasiopungua 800 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita katika jimbo la Kivu Kaskazini linalopakana na Uganda.

Kundi hilo ambalo lilizuka katika miaka ya 1990 kama vuguvugu la waasi wa kiislamu wa Uganda ni miongoni mwa zaidi ya makundi 100 ya wanamgambo yanayoendesha operesheni za kijeshi kwenye majimbo ya mashariki ya DRC.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *