img

Wanajeshi wa Iraq washambuliwa na kundi la kigaidi la DAESH wakati wa operesheni

December 13, 2020

Mwanajeshi 1 wa Iraq ameripotiwa kufariki na wengine 2 kujeruhiwa kwenye shambulizi la bomu lililotekelezwa na kundi la kigaidi la DAESH katika mji wa Kerkuk nchini Iraq.

Jeshi la Iraq liliendesha operesheni dhidi ya kundi la kigaidi la DAESH katika eneo la karibu na wilaya ya Dibis ya mjini Kerkuk.

Katika operesheni hiyo, wakati wa kuingia kwenye maficho yanayotumiwa na wanamgambo wa kundi la kigaidi, bomu lililokuwa limetegwa hapo awali lililipuka.

Mkuu wa idara ya polisi ya Kerkuk Ali Kemal, alitangaza kuwa mwanajeshi 1 aliuawa na wengine 2 walijeruhiwa kutokana na bomu hilo lililolipuliwa kwa kutumia kidhibiti cha mbali.

Kufuati shambulizi hilo, operesheni kali imeendelezwa katika eneo hilo.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *