img

“Wahitimu Maendeleo ya Jamii msichague kazi ” Dkt. Jingu

December 13, 2020

Katibu mkuu wizara ya afya , idara kuu ya maendeleo ya jamii,Dokta John Jingu amewataka wahitimu wa taaluma ya maendeleo ya jamii kubuni mbinu mbalimbali za kuweza kujiajiri badala ya kuchagua kazi ili waweze kuleta mbadiliko chanja katika jamii. 

Dr Jingu aliyasema hayo jana wakati akizungumza katika mahafali ya 11 ya wahitimu wa kozi za maendeleo ya jamii katika ngazi ya astashahada na stashaha kwa wahitimu zaidi ya 770 mahafali yaliyofanyika katika  chuo cha maendeleo ya jamii Monduli. 

Dokta Jingu ,aliwataka wahitimu hao kufikiria nje ya boksi na kujiajiri katika shughuli mbalimbali , badala ya kusubiria kupata kazi waliyosomea badala yake watumie elimu waliyoipata kama fursa  na kutochagua kazi . 

Aidha aliwaasa kuleta matokeo chanja katika jamii inayowazunguka kupitia elimu waliyoipata kwa kuhakikisha wanatatua changamoto zinazowakabili wananchi na kuweza kuleta ufumbuzi. 

“naombeni sana ndo mmehitimu kozi zenu Sasa hivi msiende kukaa tu mkisubiria kuajiriwa katika fani ya maendeleo ya jamii ,badala yake mjiongeze kwa kujiajiri huku mkileta matokeo chanja katika jamii na kuleta majawabu ya changamoto kwa jamii kwa kile mlichosomea.”alisema Dokta Jingu.

Naye Mkuu wa chuo hicho,Elibariki Ulomi alisema kuwa chuo hicho ambacho kimeanzishwa mwaka 1977 kimekuwa kikitoa elimu katika fani hiyo ambapo kimetoa wanavyuo wengi ambao wameweza kujiajiri na hata kuajiriwa katika ngazi mbalimbali.

Ulomi alisema kuwa,pamoja na kuwepo kwa mafanikio mbalimbali wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya miundombinu ambapo wana uhitaji wa vyumba vya mihadhara vitatu,mabweni 3 pamoja na watumishi katika nyanja mbalimbali wapatao 11. 

Hivyo waliomba kuboreshewa miundombinu chuoni hapo ili kuweza kupata wanafunzi wengi zaidi kulingana na uhitaji uliopo. 

Naye Mbunge wa Monduli,Freddie Lowassa alisema kuwa ,chuo hicho kimekuwa msaada mkubwa  kwa jamii ya wananchi wa Monduli  na mikoa mingine kutokana na elimu inayotolewa kuwa bora na yenye kutoa wataalamu waliobobea zaidi. 

Fredy aliwaasa wahitimu hao kutumia mitandao ya kijamii vizuri kwa kuelimisha jamii badala ya kuitumia vibaya ambayo mwisho wa siku huchangia kupotosha jamii endapo itatumika tofauti. 

Akisoma risala ya wahitimu,Mmoja wa wahitimu alisema kuwa,uongozi mpya uliopo chuoni hapo hivi Sasa wameweza kukibadilisha chuo hicho kwa kutoa elimu shirikishi ambayo itawawezesha wao kuweza kujiajiri na hata kuweza kuajiri wengine. 

Aidha alisema kuwa,kwa sasa hivi nafasi ya ajira ni chache sana hivyo wanashukuru serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya kuweza kujiajiri ,hivyo aliomba vyuo mbalimbali kuongeza wigo wa kuweza kuwaunganisha wahitimu na fursa mbalimbali za ajira.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *