img

TANESCO kuwakatia umeme wadaiwa sugu

December 13, 2020

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwakatia umeme wadaiwa wote sugu wa umeme nchi nzima bila kujali taasisi binafsi wala taasisi za umma huku akiwataka wakurungezi wote kuhakikisha wanakusanya mapato kutoka kwa wateja wao.

Dkt. Kalemani ameyasema hayo katika kikao kazi cha kwanza kilichojumuisha Wakuu wa Bodi, Menejimenti, Idara, Vitengo na Taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kilichofanyika katika ofisi za wizara zilizopo Mji wa kiserikali Mtumba Dodoma kilichokuwa na lengo la kufahamiana na kutoa maagizo na maelekezo mbalimbali. 

“Nimewaita kwa mambo mawili tu, jambo la kwanza ni kufahamiana ndilo jambo lililonifanya niwaite wajumbe wa bodi zote za wakurugezi na menejimenti pamoja na uongozi wa wizara na kufahamishana mambo ya msingi ya kufanyia kazi na jambo la pili ni kuwataarifu kuwa tumeanza kufanya kazi na kikao hiki sio kikao tu bali ni kikao cha kwanza cha kazi,” amesema Dkt. Kalemani. 

Dkt. Kalemani ameongeza kuwa, “Lazima TANESCO tukusanye mapato kutoka kwa wateja wetu maana jana nilipoingia ofisi nimepokea taarifa mpaka sasa tunadai zaidi ya  shilingi bilioni 182 kwa taasisi za umma na wateja wa kawaida shilingu bilioni 3.6, Mwenyekiti wa Bodi nakuagiza kwa tunaemdai kata umeme, acha nilaumiwe mimi kwanza, kwa hiyo kuanzia leo kama kuna mteja au taasisi iwe ya umma au ya binafsi tunayoidai naelekeza Bodi ya TANESCO kateni umeme kuanzia leo”

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *