img

Mwakamo aunda Kamati ya Mfuko wa Jimbo

December 13, 2020

Na Omary Mngindo, Mlandizi.

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Michael Mwakamo, Des 11 ameunda Kamati ya Mfuki wa Jimbo, itayosimamia shughuli za kimaendeleo jimboni humo.

Mwakamo ametangaza Kamati hiyo baada ya zoezi la kuapishwa kwa Madiwani wa Halmashauri, zoezi lililokuwa chini ya Katibu Tawala Sozi Ngate, Mkurugenzi Mtendaji Butamo Ndalahwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani hapa.

Alisema kuwa Kamati hiyo itayokuwa na Mansour Kisebengo Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri hiyo, anataraji kwamba atatumia uzoefu wake wa miaka kumi ya katika Halmashauri ili kupatikana kwa maendeleo kwenye sekta mbalimbali.

“Katika Kamati hii mbali ya diwani Kisebengo, pia atakuwepo Rehema Chuma diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Ruvu, na makatibu Kata wawili, Hilda Kivinge Kata ya Mtongani na Bhaton Mwisela Kata ya Kwala,” alisema Mwakamo.

Aliongeza kuwa kuhusu taasisi itayoingia katika Kamati hiyo ataitangaza baada ya kumbukumbu za kiofisi, ili kubaini inayofanyakazi kwa ufanisi na Halmashauri hiyo, na kwamba lengo kuu ni kuhakikisha malengo yaliyokwekwa yanafikiwa.

Akizungumzia uteuzi huo, Kisebengo alisema kwamba ameupokea kwa mikono miwili na kwamba akishirikiana na wajumbe wanaounda Kamati wana uhakika watatekeleza malengo hayo kwa ufanisi mkubwa, ili Jimbo liendelee kuwa na mafanikio.

“Nashukuru kwa uteuzi huu katika Kamati ya Mfuko wa Jimbo, kwanza nampongeza Mbunge Mwakamo kwa kuona ninatosha kuungana kwenye Kamati, niwahakikishie wana-Kibaha Vijijini kwamba tutashirikiana ipasavyo ili malengo yafikiwe,” alisema Kisebengo.

Kwa upande wake Rehema alisema kwamba pamoja na uchanga wake katika udiwani, anaimani kubwa kwamba atachangia kwa kiwango kikubwa katika mchakato huo ili mwisho wa siku wana-Kibaha wanufaike na Mfuko huo.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *