img

Msikiti uliopewa jina la ‘Yesu Kristo’ wavuta hisia za wengi mitandaoni

December 13, 2020

Dakika 10 zilizopita

Mvutano baina ya pande mbili ulikuwepo kwa miongo kadhaa

Ilianzia katika mvutano wa kisheria kati ya jumuia ya Kiislamu na Kanisa la Waadventista wa Sabato (SDA) kuhusu umiliki wa ardhi.

Mvutano huo uliokuwepo kwa miongo kadhaa, ulimalizika mwezi Oktoba mwaka huu na Mahakama ya Mazingira mjini Kisumu iliamua kuwa ardhi hiyo ni milki ya Jamii ya Kiislamu.

Katika jitihada za kujenga daraja la mahusiano kati ya jamii ya Kiislamu na kanisa, imechagua jina la msikiti ambalo limevuta hisia za wengi katika mitandao ya kijamii.

Msikiti ambao umejengwa kwenye ardhi iliyokuwa kwenye mgogo eneo la Kaloleni katika Kaunti ya Kisumu unaitwa ‘Msikiti wa Yesu Kristo mwana wa Maria ( The Mosque of Jesus Christ the son of Mary)

Lakini kwa nini jina hili la kipekee?

Abdul Rashid ni Mwadhini ameliambia gazeti la The Standard la Kenya kuwa ” Tumekuwa na mvutano wa muda mrefu kuhusu ardhi na hii ni moja ya sababu zilizotufanya kuchagua jina hili. Sisi hatuna uadui na Wakristo,” alisema.

Amesema kuwa Waislamu pia wanaamini Yesu na kuwa alikuwa sambamba na manabii wanne akiwemo Mtume Muhamad (S.A.W).

”Waislamu wanaamini katika Yesu Kristo . Uchaguzi wa jina pia ni shukrani ya Yesu Kristo ambaye tunaamini atarudi tena,” Rashid aliliambia gazeti la The Standard.

Hatua hii imegusa hisia za watu nchini Kenya wengine wakihoji je, huu ni Msikiti na Kanisa kwa wakati mmoja? Wengine wameifurahia hatua hiyo

Mipango ya kujenga msikiti wa kudumu inaendelaa ingawa Waislamu wanaoabudu kwenye eneo hilo wamejenga jengo la muda mfupi kwa ajili ya kuswali.

Baadhi ya waumini wa Kikristo wamepokea kwa mikono miwili hatua hii wakisema kuwa itajenga hali ya kuishi kwa amani.

Hili si tukio geni hata hivyo kwani jina la The Mosque of Jesus Christ” limepewa pia Msikiti ulio katika mji wa Madaba, Kusini mwa mji mkuu wa Amman huko Jordan, Msikiti huu ulianzishwa mwaka 2008 kwa ajili ya kutoa ujumbe wa umoja na kustahimiliana miongoni wa dini hizo mbili.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *