img

Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube kurejea nchini leo

December 13, 2020

Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube, aliyeenda Afrika Kusini kwa matibabu anatarajia kurudi nchini leo Desemba 13, 2020.

Dube ataondoka mjini Cape Town, saa 8:20 mchana, kwa ndege ya shirika la Kenya Airways, itayowasili Dar Es Salaam saa 5:45 usiku.

Aliondoka nchini Novemba 29 kwenda mjini Cape Town, Afrika Kusini, kufanyiwa upasuaji wa mkono wake wa kushoto alioumia na kuvunjika Novemba 25 kwenye mchezo dhidi ya Yanga SC uliomalizika kwa Yanga kushinda 1-0.

Dube alivunjika mfupa wa Ulna, unaoanzia kwenye kiwiko hadi kidole cha mwisho cha mkono.

Alhamisi ya Disemba 3, alifanyiwa upasuaji uliofanikiwa, na anatarajia kujiuguza kwa majuma manne, kabla ya kurudi uwanjani.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *